Meya mstaafu wa jiji la Arusha Kalist Lazaro akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha (Happy Lazaro).
******************************
Happy Lazaro,Arusha.
Arusha.Meya mstaafu wa jiji la Arusha ,Kalist Lazaro amemuandikia barua ya shukrani Mheshimiwa Rais John Magufuli kwa miradi mikubwa aliyoileta jiji la Arusha ikiwemo miradi ya maji, barabara,afya na miundombinu ya barabara.
Ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha,na kusema kuwa katika awamu hii ya tano inayoongozwa na Rais Magufuli amefanya mambo makubwa Sana ya maendeleo kwa jiji la Arusha ambayo anahitaji kupongezwa kwani ni mambo makubwa .
Meya alisema Rais Magufuli ni Rais asiyependa kubagua vyama vya upinzani huku akisisitiza kuwa ingawa Arusha ilikuwa inaongozwa na wapinzani lakini hakusita kuleta miradi mbalimbali ya kimaendeleo ambayo kwa sasa Jiji hilo na Mkoa mzima inajivunia.
“Nimeandika barua ya kumpongeza Rais Magufuli kwa maendeleo aliyoyafanya jijini Arusha,pamoja na kuandika kitabu chenye kurasa 78 kwa ajili ya kumpongeza Rais John Magufuli kwa kazi alizotufanyia wan Arusha na tunamuhakikishia katika uchaguzi mkuu huu tutachagua chama cha Mapinduzi “alisema Kalisti.
“Nilipokuwa Meya kabla ya kuacha nafasi hiyo mwaka huu ukweli tulikuwa tunatekeleza Ilani ya CCM hata kama tulikuwa wapinzani na mimi kama Meya wa zamani sikusita kushiriki katika shughuli za kimaendeleo ingawa wenzangu hawakunielewa awali wa chadema lakini sasa nashukuru wameelewa na kuondoka baadhi yao kuja CCM. “alisema Kalisti.
Lazaro aliongeza kuwa, katika uongozi huu wa awamu ya tano Rais Magufuli amefanya mambo makubwa Sana ya maendeleo ambayo yameliweka jiji Hilo katika hali ya maendeleo na kuondokana na changamoto mbalimbali zilizokuwa zikiwakabili.
Alisema kuwa, anampongeza jinsi alivyoweza kupambana na ugonjwa wa Corona kwa kutokubali kutufungia ndani na kumpongeza kwa hotuba nzuri aliyoitoa wakati wa kufunga bunge kwa sababu ikisheheni mambo mbalimbali na amemaliza kila kitu katika hotuba ile kwani kama ni hospitali zimejengwa, maji wananchi wanayo na huduma mbalimbali za kijamii
Alisisitiza kuwa Arusha inaahidi kupiga kura za kishindo katika uchaguzi mkuu ujao kwani sasa hivi kila mtu ameeelewa maana ya uongozi wa Rais Magufuli huku akiongezea kuwa Jiji la Arusha chini ya uongozi wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji hilo, Dk, Maulid Madeni na Mkuu wa Wilaya hiyo, Gabriel Daqqaro walisimamia mambo mbalimbali ya kimaendeleo ikiwemo kuhakikisha wanaokoa zaidi ya sh, bilioni 4.6 kwa ajili ya watumishi hewa.
Mwisho