…………………………………………………………………………
NA FARIDA SAIDY,MOROGORO.
KATIKA kuhakikisha Huduma ya umeme inafikia vijiji vyote nchini serikali imetenga Trioni moja nchi nzima kupitia wakala wa umeme vijijini(REA) huku Mkoa wa Morogoro ukitengewa zaidi ya Shilingi Bilioni 42.0 kwa ajili ya huduma hiyo kwenye Vijijini 85 katika awamu ya tatu mzunguko wa kwanza na kuwa vijiji hivyo vimeshafikiwa na ifikapo Mwezi Julai mwaka huu vijiji 165 vitakuwa vimepata umeme.
Kauli hiyo imetolewa na Kamishna Msaidizi wa umeme toka Wizara ya Nishati Mhandisi Inocent Luoga,wakati akikagua mradi wa umeme vijijini amesema kuwa huduma hiyo itafikia pia wananchi katika vitongoji vilivyopo kwenye Vijiji hivyo.
Kwa upande wake Mhandisi Gasper Lyimo kutoka kampuni ya State Grid inayojenga umeme vijijini katika mkoa wa Morogoro amewahakikishia Wananchi wa Kijiji cha Vidunda kuhakikisha wanakamilisha Mradi huo kwa wakati na kuomba ushirikiano toka kwa Wananchi.
Aidha Diwani wa Kata ya Vidunda Bw Godian Makoye,ameahidi kushirikiana na kampuni hiyo kufanikisha mradi kwa kushirikisha wananchi kujitokeza kwa nguvu kazi ya kubeba nguzo hadi maeneo husika.
Nao Wananchi wa Kata hiyo wamepongeza hatua hiyo kwa kuwa itasaidia kuleta maendeleo katika Kijiji hicho kwani huduma hiyo waliokuwa wakiisubiri kwa muda mrefu.
Ziara hiyo imeshirikisha watendaji kutoka shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania(Tanesco) likiongozwa na Naibu Mkurugenzi wa shirika hilo ,wakala wa umeme vijijini(REA)na maafisa kutoka wizara ya Nishati ambapo watetembelea miradi ya umeme vijijini katika wilaya za Kilosa,Ulanga,Kilombero,Mailinyi,Gairo,Mvomero .