Mjumbe wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Henry Mwimbe (kushoto) akikagua vifaa vya ujenzi wa Umeme vya mradi wa Kampuni ya kusambaza Umeme ya Ccce Co Ltd inayo sambaza umeme vijiji vya Wembere na Ntwike wilayani Iramba mkoani Singida. Kulia ni Wafanyakazi wa kampuni hiyo.
Raia wa China Wafanyakazi wa kampuni hiyo wanao tekeleza mradi huo.
Majadiliano kabla ya kwenda kukagua mradi huo.
Transfomer zikiwa eneo la mradi tayari kwa kufungwa.
Mjumbe wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Henry Mwimbe (kulia) akikagua vifaa vya ujenzi wa umeme vya mradi huo.
Nguzo zikiwa eneo la mradi wilayani Iramba.
Na Ismailly Luhamba, SINGIDA.
BODI ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imesema haitasita kuwachukulia hatua za kisheria ikiwemo kuwashitaki na kuwafilisi wakandarasi watakaoshindwa kumaliza kwa wakati shughuli za usambazaji wa nishati ya umeme kwenye maeneo waliyokabidhiwa ifikapo Juni,30,mwaka huu.
Mjumbe wa Bodi ya REA, Henry Mwimbe aliyasema hayo alipokuwa akitembelea na kukagua mradi wa usambazaji nishati ya umeme vijijini katika wilaya ya Iramba unaotekelezwa na Kampuni ya Ccce Co Ltd kwenye vijiji vya Wembere na Ntwike wilayani Iramba.
Aidha Mwimbe alifafanua kwamba kutokana na mkataba walioingia na Makampuni yanayosambaza nishatai hiyo kwa hali hiyo hawatakuwa na huruma na wala hawataweza kuongeza muda wa mkataba hata siku moja na badala yake watazingatia yale waliyokubaliana kwa nujibu wa mkataba waliosaini nao.
“Na uzuri ndani ya mkataba kunaelezwa majukumu ya kila pande kwenye huo mkataba na ainaelezwa pia unaposhindwa kutekeleza kile ulichopaswa kufanya kwa mujibu wa mkataba,nini kinafuata kuna kushitakiwa pale,kuna kufilisiwa pale.”alisisitizs mjumbe huyo wa Bodi ya Rea.
Hata hivyo Mjumbe huyo wa Bodi ya Rea aliweka wazi pia kwamba kwa mtu mwenye kampuni ambayo anataka kampuni yake iende mbele kuna akutopewa kazi na kuongeza kwamba haadhani kama kuna kampuni inawerza kuendelea kujiendesha bila kazi na mteja wake mkubwa ni serikali kupitia rea kuwapatia kazi hizo.
Kaimu Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa REA, Mhandisi Elineema Mkumbo aliweka wazi kuwa katika mradi huo ambao ni wa tatu mzunguko wa kwanza unatekelezwa katika mikoa 25 ya Tanzania na lengo lilikuwa ni kupeleka katika vijiji 3,559.
Kwa mujibu wa Mhandisi Mkumbo mpaka ifikapo Juni,30 mwaka huu vijiji hivyo 3,559 viwe vimepatiwa umeme na kukamilika kwa vijiji hivyo kutakuwa kumepelekea zaidi ya asilimia 70 ya vijiji vya Tanzania kuwa na miundombinu ya umeme.
Hata hivyo wakati awamu ya tano inachukua madaraka mwaka 2016 Tanzania vijiji 2,018 vya Tanzania ndivyo vilivyokuwa na umeme na hadi kufikia Aprili,mwaka huu vijiji vilivyokuwa na umeme vilikuwa 9,200.
Kwa aupande wake Meneja Mradi wa Mradi wa Wakala wa Nishati vijijini (REA) awamu ya tatu,Mhandisi Baraka Mhagama alibainisha kwamba mpaka sasa mradi huo umefikia asilimia 90 na asilimia kumi zilizobakia ni zile ambazo zilikuwa zikikabiliwa na changamoto mbali mbali.
Alizitaja changamoto hizo kuwa ni pamoja na usafirishaji wa vifaa na kwamba kama inavyofahamaika sera ya Rais ni kwamba asilimia kubwa ya vifaa vinunuliwe ndani ya nchi.
“Asilimia kubwa ya changamoto ni katika uletaji wa vifaa kama mnavyojua sera ya Rais ni kwamba asilimia kubwa ya vifaa ichukuliwe ndani kwa hiyo kwa wasambazajai wetu wa ndani kidogo uwezo wao ulikuwa sio mzuri hasa kwa nguzo lakini tuliweza kupambana nazo na mwisho wa siku tumezipata za kutosha.” alisema Mhagama.