Riyad Mahrez akishangilia baada ya kuifungia Manchester City mabao mawili dakika za 43 akimalizia pasi ya Fernandinho na 45 na ushei kwa penalti katika ushindi wa 5-0 dhidi ya Burnley kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku wa jana Uwanja wa Etihad. Mabao mengine ya Man City yalifungwa na Phil Foden mawili pia dakika za 22 na 63 na David Silva dakika ya 51 na kwa ushindi huo, Liverpool itahitaji kushinda mechi zijazo ili kutawazwa rasmi kuwa mabingwa wapya wa England PICHA ZAIDI SOMA HAPA