Meya mstaafu wa halmashauri ya jiji la Arusha Kalist Buhay akiongea na vyombo vya habari mapema leo kumshukuru Mh.Rais Dkt.John Magufuli kwa kuleta fedha za miradi ya maendeleo pamoja na ruzuku kwa halmashauri bila kubagua itikadi za vyama zaidi ya bilion 252 .
picha na Ahmed Mahmoud Arusha
*******************************
Na Ahmed Mahmoud Arusha
Meya Mstaafu wa Halmashauri ya jiji la Arusha Kalist Lazaro amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Magufuli kwa kutoa fedha za miradi ya maendeleo kwa jiji la Arusha katika kipindi cha miaka mitano kuanzia 2015\2020 licha ya Halmashauri hiyo
kuongozwa na upinzani.
Kalist aliyasema hayo wakati akiongea na waandishi wa habari jijini Arusha na kuwataka Wana Arusha kumuunga mkono mh.Rais kwa hatua yake aliyoahidi na kuendelea kuahidi kuwa maendeleo hayana chama ambapo jumla ya fedha za ujenzi wa miradi zaidi ya Trilion 1 zimetolewa na
serikali yake.
Alisema kuwa fedha hizo ni pamoja na fedha za ruzuku maendeleo mishahara ambazo bado serikali iliendelea kuleta fedha hizo na kujengwa miradi mikubwa ya maji wa billion 520 ambao ni mkubwa na wa pili hapa nchini baada ya ule wa ziwa victoria.
“Mh.Rais nitampelekea barua ya kumshukuru kwa serikali yake kutenga fedha nyingi kwa mkoa na halmashauri yetu ipo miradi mingi inayotekelezwa ikiwemo Barabara za lami zaidi ya km.42 kwa jiji letu la Arusha Elimu bure ujenzi wa Madarasa shule za msingi na sekondari sanjari na ufaulu hizi zote ni juhudi zake katika kutekeleza ilani ya chama cha Mapinduzi”.
Aliongeza kueleza kwamba katika kuendeleza miradi ya kimaendeleo nchini Mh.Rais hakuangalia Itikadi za vyama bali aliweka maslahi ya wananchi mbele hivyo kila kona ya nchi yetu serikali imepeleka maendeleo kwa kiwango kikubwa na sote ni mashahidi na pia nawashangaa baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani kuwa serikali haijaleta
maendeleo.
“Hizi sio siasa safi bali ni kushindwa kwa kufikiri kwa viongozi waliokosa dira na maono ya kuongoza jamii siasa ni maisha ya watu hivyo kila hatua unayopiga inahitajika kuunga mkono juhudi za Yule anayetekeleza ilani ya chama kinachoongoza dola hivyo sio serikali hii imefanya kazi kubwa ya kupigiwa mfano tutakuwa wanafki kama hatuatatoa shukran zetu kwa Dkt.Magufuli”.
Aidha alielezea baadhi ya vitu alivyotekeleza kipindi akiwa Meya ni pamoja na kusababisha halmashauri ya jiji la Arusha kupata hati safi kwa kipindi chote cha awamu ya Tano,pia amesababisha mapato ya ndani kuongezeka kutoka million 700 hadi billion 17.6 huku hadi mwaka huu wa fedha kiwango hicho watafikia malengo na kuzidi.
Kwa mujibu wa Meya huyo mstaafu aliwataka viongozi wapya walipoewa dhamana juzi kuonyesha ushirikiano kwa wananchi pamoja na wafanyakazi huku akiwasisititiza kusikiliza kero na kuzitatua bila upendeleo wowote hali itakayosaidia kuwepo kwa Ari na utelekezaji wa majukumu
kwa ufanisi ili kila mmoja aweze kupata maendeleo tunayotarajia.