…………………………………………………………………
Na Masanja Mabula, Pemba.
MAHAKAMA ya Mkoa wa Kaskazini Pemba imemhukumu kijana mohd hassan mohd 19 wa junguni wete kwenda chuo cha mafunzo kwa muda miaka miwili baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kutorosha.
Kijana huyo ametenda kosa hilo tarehe 31/01/2020 huko Junguni ambapo alimbaka msichana mwenye umri wa miaka 17.
Mtuhumiwa huyo amekiri kosa baada ya kusomewa sitaka na mwendesha mashataka wa serikali Ali Amour Makame.
Hata hivyo hakimu wa mahakama hiyo abdalla yahya shamhuna amemtaka kijana huyo kulipa faini ya shiingi laki 5 pamoja na fidia ya shilingi laki 1 kwa mwathirika akishindwa aende chuo cha mafunzo kwa miaka miwili.
Wakati huo huo mahakama hiyo pia imempeleka rumande kwa muda wa wiki mbili kijana khamis shaib Khatib anayetuhumiwa kwa kosa la ubakaji.
Kijana huyo mwenye umri wa miaka 24 , mkaazi ya Kizimbani Wete anadaiwa kumbaka msichana mwenye umri wa miaka 13.
Mbele ya hakimu wa mahakama hiyo abdalla yahya shamuhun mwendesha mashtaka wa serikali mohd said mohd ameiambia mahakama kuwa mtuhumiwa huyo ametenda kosa hilo tarehe isiyofahamika ya mwezi 11/2019 majira ya saa 3 asbh , ambapo alimbaka msichana huyo mwenye umri wa miaka 13.
Mtuhumiwa huyo amepelekwa rumande hadi tarehe 6/7/2020 kesi yake itakapokuka kutajwa tena.