Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Edward Mpogolo, akijaza fomu jana za kumdhamini Rais Dk.John Magufuli anayeomba ridhaa ya chama chake kugombea urais mwaka huu. Kulia ni ,
Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ikungi, Noverty Kibaji.
Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ikungi, Noverty Kibaji, akizungumzia mchakato wa kumdhamini anayeomba ridhaa ya kugombea urais mwaka huu kupitia chama hicho Rais Dk. John Magufuli.
Wana CCM wakijaza fomu za kumdhamini mgombea wao. Kulia ni Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Ikungi, Bwanga Akida Tayari.
Fomu ikijazwa
Na Dotto Mwaibale, Singida
SIKU moja baada ya Waziri wa Mambo ya Nje mstaafu, Bernard Membe, kuzungumzia suala la mchakato wa kumpata mgombea urais ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Edward Mpogolo amejitokeza na kumjibu.
Akizungumza jana wakati wa hafla ya wanachama wa CCM Ikungi waliojitokeza kumdhamini Rais Dk.John Magufuli anayeomba ridhaa ya chama chake kugombea urais, alisema Membe alipata wapi kibali cha kuitisha mkutano na kuzungumza na wananchi.
” Ndugu zangu waandishi wa habari niseme tu kwamba nashukuru kwa kuniuliza swali ili nimeisikiliza hiyo clip zaidi ya mara nne ili nami niweze kujifunza ni alikuwa anataka kusema. Kwa kweli sikupaswa kuijibu lakini kwa sababu ya baadhi ya vitu katika mazungumzo yake yananiwia na mimi kama kijana kujibu vitu ambavyo vinasababisha na mimi kuwa sehemu ya kujibu kile alicho kisema mzee Membe ni mambo machache.
Mpogolo alisema kwanza katika clip yake amewataja vijana Tanzania na yeye ni sehemu ya vijana wa Tanzania.
Alisema katika clip hiyo amezungumzia suala la kuiambia Tanzania na dunia na yeye ni sehemu ya dunia na Tanzania lakini sio sehemu ya kujibu kutokana na chama au nini lakini ni kama tu sehemu ya vijana na Mtanzania na sehemu ya mkazi wa dunia.
Alisema katika clip hiyo Membe amesema amepigiwa simu nyingi sana kutoka kona mbalimbali za Tanzania jambo ambalo pia limemfanya aweze kuchangia kujibu.Lakini kauli nyingine ambayo pia inamfanya aweze kusema chochote au kujiuliza ni ile aliyosema chochote kinaweza kikatokea hapa katikati sasa yeye kama mkuu wa wilaya katika eneo lake anaanza kutafakari ni kitu gani hicho kinachoweza kutokea ukizingatia kwamba Membe ni Mzee aliyekuwa kwenye uongozi kwa muda mrefu anasema hivyo na yeye kama ni mwenyekiti wa kamati ya usalama kwenye eneo lake anajiuliza ni kitu gani hicho kitakachoweza kutokea ndio maana ameona naye awe sehemu ya kumjibu.
Alisema eneo jingine alilo ongea ni kuwa anaogopa kuingia kwenye mitego ni mitego gani hiyo ni maana akaona akiwa kama kijana wa Tanzania akaona anapaswa kumjibu badala ya kukaa kimya ambapo linaweza likaenezwa na dunia ikamwamini.
” Kabla ya kumjibu nimekuwa na maswali ya kujiuliza nimeona Membe amefanya kama mkutano hivi lakini swali langu ambalo najiuliza nani amempa kibali cha kufanya mkutano katika kipindi hiki tuna corona na je kama alipewa kibali nani alimuandalia mkutano na swali lingine ninalo jiuliza je ni nani mzee Membe kitendo cha kuandaliwa mkutano je ni Mbunge au ni nani na kwanini afanye mkutano wakati hakuna ruhusa ya mikutano ni maswali ambayo yananifanya niwe sehemu ya mjadala.” alisema Mpogolo.
Mpogolo alisema anajiuliza Membe anasema pia ana mitego kama kijana alijiuliza ni mitego ipi mzee amesha staafu yupo nyumbani ni mitego gani hiyo ambàyo anaiogopa na ni nani huyo anàye muingiza kwenye hiyo mitego?
Mpogolo aliongeza kuwa swali lingine analo jiuliza ni kuwa Membe anazungumzia Tume Huru ya uchaguzi wakati wote ambao alikuwa kwenye nafasi za uongozi ndani ya chama na Serikalini mbona hakuwahi kuzungumzia iweje leo huyo mzee inaonesha anazeeka vibaya anapaswa kuzomewa.
Mpogolo alisema viongozi wa Mkoa wa Lindi wanapaswa kuulizwa kuhusu mkutano huo ambao inaonesha ulikuwa batili na akahoji kwa nini mpaka sasa Membe awe
mtaani badala ya kuwa amekamatwa.
Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ikungi, Noverty Kibaji akizungumzia mchakato wa udhamini wa mgombea urais kupitia chama hicho Mhe. John Magufuli alisema wanaccm wengi wamejitokeza ambapo mpaka jana jioni wamefikia 175 zaidi ya 150 kulingana na takwimu za kitaifa na kuwa bado wanachama wengine wamekuwa wakiendeleankujitokeza kumdhamini mgombea huyo.