Home Siasa CCM KAMATI YA SIASA YA WILAYA TANGA WAJIPANGA VYEMA KUELEKEA UCHAGUZI MKUU...

CCM KAMATI YA SIASA YA WILAYA TANGA WAJIPANGA VYEMA KUELEKEA UCHAGUZI MKUU 2020

0
……………………………………………………………………………..
Na. Alex Sonna
Kamati za siasa za kata, viongozi wote wa matawi na viongozi wa Jumhuiya zote za Chama Cha  Mapinduzi wilaya ya Tanga wametakiwa kujitathimini  na ushindi wa uchaguzi 2020 ili kupata mafanikio zaidi.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu wa Siasa na Uenezi wilaya ya Tanga, Ndg. Lupakisyo Kapange leo katika Semina ya kujipima ili kupata ushindi katika uchaguzi wa 2020.
Aidha semina hiyo ilipata baraka za Waziri wa afya, Mjumbe wa Kamati ya siasa wilaya ya Tanga na Mbunge mlezi chama wilaya ya Tanga. 
 Katika semina hiyo akitoa salamu Mhe. Ummy Mwalimu amewashukuru wana CCM , wanatanga na viongozi wa Dini kwa kumuombea kwa mwenyezi Mungu katika kipindi chote cha utumishi wake.
 “ malezi mliyonipa wanatanga yamemfanya kufanyakazi kwa bidi,”Mhe. Ummy
Akizungumza Mhe. Ummya Mwalimu amesema kuwa Mhe. Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya kazi kubwa katika Taifa hili  hivyo amesema namna nzuri ya kumshukuru Mhe. Rais kwa kazi nzuri aliyotufanyia wanatanga ni kuhakikisha kuwa tunampigia kura za NDIYO za kishindo kuanzia 90% – 100%.  
Katika hatua nyingine Wanasemina wamepata nafasi ya kusafishiana nia kwa kusameheana ili kuhakikisha wanakuwa kitu kimoja na malengo ya chama chao yananapatikana kwa ushindi wa kishindo katika uchaguzi wa 2020.
Semian hiyo imehusisha kata za Kata Chumbageni, Kata Maweni na Kata Nguvumali
Ratiba ya semina Inaendelea kesho kwa kata zingine.