Home Mchanganyiko SERIKALI YAITAKA JAMII KUHAKIKISHA WATOTO WANAPATIWA CHANJO KUONGEZA KINGA

SERIKALI YAITAKA JAMII KUHAKIKISHA WATOTO WANAPATIWA CHANJO KUONGEZA KINGA

0

Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma ya Afya ya Uzazi na Watoto, Dk.Ahmad Makuwani akizungumza na waandisi wa habari (hawapo pichani) wakati wa  semina ya waandishi wa habari wa mikoa ya Singida na Dodoma kuhusu chanjo iliyofanyika jijini Dodoma.

Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma ya Afya ya Uzazi na Watoto, Dk.Ahmad Makuwani akisisitiza jambo kwenye semina ya waandishi wa habari wa mikoa ya Singida na Dodoma kuhusu chanjo iliyofanyika jijini Dodoma,kulia ni Mratibu wa huduma za chanjo mkoa wa Dodoma Dkt.Paul Mageni ambaye alimuwakilisha Mganga Mkuu wa Mkoa huo.

Ofisa Programu ya chanjo katika Mpango wa Taifa wa Chanjo kutoka Wizara ya Afya, Bi.Lotalis Gadau,akitoa mada  kwenye semina ya waandishi wa habari wa mikoa ya Singida na Dodoma kuhusu chanjo iliyofanyika jijini Dodoma.

Mratibu wa huduma za chanjo mkoa wa Dodoma Dkt.Paul Mageni,akitoa taarifa za chanjo mkoa wa Dodoma kwenye semina ya waandishi wa habari wa mikoa ya Singida na Dodoma kuhusu chanjo iliyofanyika jijini Dodoma.

Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma ya Afya ya Uzazi na Watoto, Dk.Ahmad Makuwani (kulia) akiteta jambo na Ofisa Programu ya chanjo katika Mpango wa Taifa wa Chanjo kutoka Wizara ya Afya, Bi.Lotalis Gadau  wakati wa  semina ya waandishi wa habari wa mikoa ya Singida na Dodoma kuhusu chanjo iliyofanyika jijini Dodoma.

Baadhi ya waandishi kutoka vyombo mbalimbali wakimsikiliza Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma ya Afya ya Uzazi na Watoto, Dk.Ahmad Makuwani (hayupo pichani) wakati wa  semina ya waandishi wa habari wa mikoa ya Singida na Dodoma kuhusu chanjo iliyofanyika jijini Dodoma.

Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma ya Afya ya Uzazi na Watoto, Dk.Ahmad Makuwani (wa katikati aliyekaa) kushoto kwake ni Ofisa Programu ya chanjo katika Mpango wa Taifa wa Chanjo kutoka Wizara ya Afya, Bi.Lotalis Gadau  na kulia ni Mratibu wa huduma za chanjo mkoa wa Dodoma Dkt.Paul Mageni ambaye alimuwakilisha Mganga Mkuu wa Mkoa huo wakiwa kwenye picha ya pamoja na waandishi kutoka mkoa wa Singida baada ya kumaliza semina ya waandishi wa habari wa mikoa ya Singida na Dodoma kuhusu chanjo iliyofanyika jijini Dodoma.

Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma ya Afya ya Uzazi na Watoto, Dk.Ahmad Makuwani (wa katikati aliyekaa) kushoto kwake ni Ofisa Programu ya chanjo katika Mpango wa Taifa wa Chanjo kutoka Wizara ya Afya, Bi.Lotalis Gadau  na kulia ni Mratibu wa huduma za chanjo mkoa wa Dodoma Dkt.Paul Mageni ambaye alimuwakilisha Mganga Mkuu wa Mkoa huo wakiwa kwenye picha ya pamoja na waandishi  wa Mkoa wa Dodoma  baada ya kumaliza semina ya waandishi wa habari wa mikoa ya Singida na Dodoma kuhusu chanjo iliyofanyika jijini Dodoma.

…………………………………………………………………………………………

Alex Sonna, Dodoma

Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma ya Afya ya Uzazi na Watoto, Dk.Ahmad Makuwani ameitaka jamii kuhakikisha watoto wanapata chanjo kipindi hichi chenye maambukizi ya Virusi vya  Corona (Covid-19 ) ili wapate kinga ya magonjwa mengine.

Wito huo umetolewa leo na Dk.Makuwani wakati wa  semina ya waandishi wa habari wa mikoa ya Singida na Dodoma iliyohusu chanjo iliyofanyika jijini Dodoma.

Aidha Dkt. Makuwani amesema kuwa  maambukizi ya Corona kwasasa yamepungua na kuwataka watanzania kutotumia ugonjwa huo kama sababu ya kutowapeleka watoto kupata chanjo.

“Tulikuwa tunaenda vizuri lakini hivi karibuni idadi ya watoto na wasichana wanaopaswa kupata chanjo ya mlango wa kizazi imepungua, hizi chanjo ni muhimu sana jamii ipeleke watoto kwenye vituo wapate chanjo,”ameeleza Dkt. Makuwani

Hata hivyo Dkt. Makuwani ameeleza kuwa Tanzania imepiga hatua kwasasa katika utoaji wa huduma za chanjo huku akisema  kuwa kuna vituo zaidi ya 600 vinavyofanya uchunguzi wa saratani ya mlango wa kizazi.

“Tunaamini mtatumia weledi wenu kuelimisha jamii kuhusu huduma ya chanjo mbalimbali zinazotolewa, wahimizeni wananchi kule vijijini wapeleke watoto wao kwa kuwa chanjo inatolewa kwenye vituo vya kutolea huduma,”amesisitiza Dkt. Makuwani.

pia ametoa wito kwa  waandishi kuendelea kuhamasisha wananchi kunawa mikono kwa kuwa imesaidia kuondokana na magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindupindu.

Naye  Ofisa Programu ya chanjo katika Mpango wa Taifa wa Chanjo kutoka Wizara ya Afya, Lotalis Gadau, amesema kuwa  pamoja na jitihada za kuhakikisha magonjwa yanayizuilika kwa chanjo yanapewa kipaumbele kwa kuwapatia watoto chanjo lakini bado kuna jamii hazichanji watoto.

“Kuwepo kwa ugonjwa wa Corona sio sababu ya kutopeleka watoto kupata chanjo kwasababu wakichanjwa inasaidia kuwakinga na magonjwa mengi zaidi,”ameongezea Gadau.

Amebainisha Gadau kuwa chanjo ya Surua, Rubella na HPV ya kuzuia saratani ya mlango wa kizazi uchanjaji wake upo kwa kiwango cha chini na kuwataka waandishi wa habari kuhamasisha jamii.

Kwa upande wake Mratibu wa huduma za chanjo mkoa wa Dodoma Dkt.Paul Mageni,amesema kuwa kwa sasa tumetoka kwenye janga la Corona na hali ni nzuri lakini tusijisahau popote tulipo tuendelee kuzingatia tahadhari zote zinazotolewa na Wizara ya Afya pamoja na Serikali kwa ujumla.

”Kila mwaka kitaifa huwa tunafanya mwezi wa nne chanjo ya kinga zetu na mwaka huu hatujafanya hivyo tumeamua kuwaita nyie waandishi wa habari ili mkatoe Elimu kwa jamii na kuwahamasisha wapeleka watoto wao wakapate chanjo”amesema Dkt.Mageni

Hata hivyo Dkt.Mageni amesema kuwa chanjo ya mlango wa kizazi zipo chini  kutokana na walengwa wake wapo katika jamii na mkumbuke kuwa shule zilifungwa hivyo haikuwa rahisi kuwapata wa kwetu ila kwa sasa hali ni safi na nyie mtatusaidia kutoa elimu ili waweze kuwapeleka au wahusika waende katika maeneo ili wakapate chanjo.