***********************************
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es salaam Cathy Kamba Amepokea Maandamano ya Wanachama wa Shirikisho la Vyama Vya Waendesha Bodaboda Mkoa Dar es salaam, ambao wamefanya Shughuli Mbalimbali za kuonyesha Shukrani kwa Serikali ya Awamu ya Tano Chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli ikiwa ni pamoja na kutembelea Miradi ya kimkakati iliyotekelezwa na Serikali.
Aidha Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe.Paul Makonda amewapongeza Waendesha Bodaboda hao na kuwaahidi kuwa nao pamoja katika kulinda maslahi yao na kuwaomba wawe walinzi namba moja wa amani ya Mkoa wa Dar es salaam.
Mhe.Makonda ametumia Fursa hiyo kuwataka waendesha boda boda wajitokeze kuwania nafasi mbalimbali kupitia Chama Cha Mapinduzi kuelekea uchaguzi Mkuu 2020, “Chama Cha Mapinduzi hakina ubaguzi na ndio Chama pekee ambacho unaweza kupata nafasi bila ya pesa wala konekisheni”
Kwa niaba ya Madereva Bodaboda hao Mwenyekiti wa Vyama Hivyo Ndg.Edward Mwinyisongole amesisitiza kuwa wanashukuru kwa kuruhusiwa kuingia Mjini ambao ilikuwa changamoto kwao lakini pia ameiomba serikali ya Chama Cha Mapinduzi kuendelea kutatua baadhi ya changamoto zinazoendelea kuwakabili kama ushuru wa maegesho unaotozwa na TARURA, Ubovu wa Mikataba yao na Waajiri wao pamoja na Kero kwa baadhi ya askari wasio waadilifu.
Pia Shirikisho la Vyama Vya Waendesha boda boda wamepongeza kazi nzuri inayofanywa na Serikali ya awamu ya Tano na wamekabidhi zawadi ya Tuzo kwa Rais Dkt.John Magufuli kama Shukrani kwa kuwajali waendesha Boda boda na Makundi mengine ya Wafanyabiashara Wadogo Wadogo.