Na Humphrey Shao, Dar es Salaam
Tasisi isiyo ya Kiserikali ya Haki
Elimu Tanzania imesema katika kipindi hiki cha shule kufungwa nje ya utaratibu
rasmi wa likizo kimetufanya tugundue namna mfumo wetu wa utoaji elimu ulivyo na
mapungufu mengi.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Shirika
Hilo Dk.John Kalaghe alipokuwa akizungumza na wadau wa elimu kupitia mkutano
uliandaliwa na tasisi hiyo uliofanyika kwa njia ya mtandao wakati wa
mahadhimishoi ya siku ya mtoto wa Afrika.

Dk Kalaghe alisema kuwa hofu iliyooneshwa
na Serikali, wazazi, na wadau wengine wa elimu kuhusu hatima ya ujifunzaji na
ufundishaji inatoa picha halisi ya namna mfumo wetu wa ujifunzaji na
ufundishaji ulivyojifungia kwa sehemu kubwa katika kuta za madarasa peke yake.

“Barani Afrika, hatari ni kubwa zaidi
kwa kuwa hali ya upatikanaji wa elimu ina changamoto nyingi hata kabla ya
maambukizi ya virusi vinavyosababisha COVID 19. Katika Ukanda wa Kusini mwa
Jangwa la Sahara mathalani, hata kabla ya shule kufungwa takribani 1 ya 5 ya
Watoto wa umri wa miaka 6 mpaka 11 hawakuwa shuleni; 1 kati ya 3 ya watoto wa
umri wa miaka 12 hadi 14 nao pia hawakuwa shuleni huku takribani asilimia 60 ya
vijana wa umri wa miaka 15 hadi 17 wanaopaswa kuwa shule za sekondari hawakuwa
shuleni. Nchini Tanzania, (UNICEF) zaidi ya Watoto Milioni mbili wa umri wa
shule ya Msingi na zaidi ya Watoto Milion 1.5 ya Watoto wa umri wa kuwa shule
za Sekondari, Hawako Shuleni.” Alisema Kalaghe.

Alisema umuhimu wa watoto kuwa shuleni
na kujifunza hauhitaji kupigiwa mbiu, bali ni zile athari na hasara za wao kuwa
nje ya mifumo rasmi ya kujifunza. Hapa kwetu Tanzania, pamoja na kufunguliwa
kwa Vyuo na kuruhusiwa kwa wanafunzi wa Kidato cha Sita kuendelea na mitihani
yao ya mwisho; bado takribani wanafunzi milioni 12 wa ElimuMsingi wanaendelea
kubaki nyumbani kwa Mwezi wa Tatu sasa tangu uamuzi wa kusimamisha masomo
ulipotolewa Tarehe 17, Machi 2020.

Anataja kuwa kipindi hiki cha shule
kufungwa nje ya utaratibu rasmi wa likizo kimetufanya tugundue namna mfumo wetu
wa utoaji elimu ulivyo na mapungufu mengi. Hofu iliyooneshwa na Serikali,
wazazi, na wadau wengine wa elimu kuhusu hatima ya ujifunzaji na ufundishaji
inatoa picha halisi ya namna mfumo wetu wa ujifunzaji na ufundishaji
ulivyojifungia kwa sehemu kubwa katika kuta za madarasa peke yake.

“Mijadala iliyoibuka kuhusu njia
mbadala za kuendelea kujifunza na kumlinda mtoto wakati wa kipindi hiki cha
COVID-19, ni ushahidi tosha wa namna ambavyo mfumo wetu wa utoaji elimu ulivyo
nyuma ya wakati. Mathalani, moja ya njia mbadala iliyotiliwa mkazo ni matumizi
ya vipindi vya Televisheni na Redio kumwezesha mwanafunzi kuendelea kujifunza
akiwa nyumbani. Hata hivyo, kwa mujibu wa Utafiti wa Bajeti za Kaya (Household
Budget Survey, 2017-2018, asilimia ya nyumba ambazo zina redio, televisheni na
simu ni 43%, 24% na 78% mtawaliwa (respectively) pekee.”

Alisema Pamoja na ukweli kwamba idadi
ya watanzania wenye uwezo wa kusikiliza vipindi vya redio na televisheni
kupitia simu janja na simu za kawaida, unaongezeka, lakini bado idadi hii
inaonesha siyo kaya zote zinaweza kutumia njia hizi kwa watoto wao kutokana na
kutokuwa na uwezo wa kumiliki njia hizi za mawasiliano. Hii ina maana kwamba
njia hizi, pamoja na changamoto zake, bado ni njia ambazo haziwezi kuwafikia
wanafunzi wote hasa wanaotoka kwenye familia maskini.

“Mapendekezo ya kutumia teknolojia hasa
ya kimtandao nayo ina mapungufu yake pamoja na kuwa ni njia muafaka. Ukiachilia
mbali ujuzi mdogo wa wazazi, walimu na wanafunzi kwenye namna ya kutumia
teknolojia ya mtandao na vifaa vyake kama kompyuta/tarakilishi na simu; bado
idadi kubwa ya wanajamii hawana uwezo wa kununua vifaa na kugharamia bando
zinazowezesha mtandao kuwepo. Kwa mfano, kulingana na ripoti ya Mamlaka ya
Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) ya Disemba, 2019, Tanzania ilikuwa na
jumla ya watumiaji wa mtandao 25,794,560 ambayo ni 46% tu ya soko au watu
wanaotarajiwa kutumia mitandao.

Wastani wa gharama za matumizi ya
intaneti bado uko juu pia; kwa wastani angalau MB 75 ni Tshs 1,000 kwa siku,
sawa na Tshs 30,000 kwa mwezi. Ni familia chache sana zinazoweza kugharamia au
kutenga kiasi hiki cha fedha kwa mwezi kwa ajili ya mtandao pekee. Kwa sababu
hii, njia hizi pia ni wazi kuwa zitazidi kuwaacha pembeni sehemu kubwa ya
wanafunzi ambao wengi wanatoka familia maskini na wanaosoma shule za umma.”
Alisema Kalaghe

Alisema kwa bahati mbaya, utamaduni
wetu wa utoaji elimu haumfanyi mzazi au mlezi kuwa sehemu kuu ya kujifunza kwa
mtoto. Ni nadra sana shule zetu, hasa za umma, wameweza kujenga utamaduni wa
kutoa kazi za kufanyia nyumbani kwa watoto (homework) ambazo anatakiwa kufanywa
kwa pamoja na wazazi nyumbani. Hii inasababisha hatari zaidi kwa mwanafunzi
kuwa nyumbani kwa kuwa anakosa uhakika wa kuendelea kujifunza kupitia wazazi au
walezi.

Pamoja na taarifa za UNICEF 2011,
kuonesha kuwa matukio mengi ya unyanyasaji wa Watoto yanatokea shuleni na
njiani kutoka ama kwenda shule; taarifa za hivi karibuni za Kituo cha Sheria na
Haki za Binadamu (LHRC, 2019) zinaonesha pia kuwa matukio haya yanatokea
nyumbani. Mfano kwa mujibu wa ripoti ya LHRC 2019 kati ya Mwaka 2018 na 2019 kesi
zaidi ya 2,540 za wanafunzi wa kike kupata mimba; matukio 3,709 ya ubakaji na 688
ya ulawiti yaliripotiwa polisi kuanzia mwezi Januari hadi Juni 2019. Sehemu
kubwa ya matukio haya yalitokea nyumbani na mitaani ambako watoto hawa
wanalazimika sasa kubaki katika kipindi cha COVID-19.