Makamu wa Askofu wa Jimbo Katoliki Shinyanga, Padri Kizito Nyanga (katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa jengo jipya la Huduma za tiba na matunzo kwa watuwanaoishi na Virusi vya Ukimwi (CTC) Juni 18, 2020 lililojengwa kwa msaada wa Shirika lisilo la Kiserikali la Doctors With Africa- CUAMM kupitia mradi wa Test and Treat; katika Zahanati ya Old Maswa inayomilikiwa na Kanisa Katoliki Jimbo la Shinyanga (Kulia) Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dkt. Khamis Kulemba na (kushoto) Mratibu wa Mradi wa Test and Treat Shinyanga na Simiyu , Ndg. Franscesco Bonanome.
Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Old Maswa inayomilikiwa na Kanisa Katoliki Jimbo la Shinyanga (kushoto) akitoa maelezo ya utoaji wa huduma katika zahanati hiyo kwa viongozi mbalimbali walioshirikia katika hafla ya uzinduzi wa jengo jipya la Huduma za tiba na matunzo kwa watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (CTC ) Juni 18, 2020 lililojengwa kwa msaada wa Shirika lisilo la Kiserikali la Doctors With Africa-CUAMM kupitia mradi wa Test and Treat (kulia) ni Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dkt. Khamisi Kulemba wa Mradi wa Test and Treat Shinyanga na Simiyu , Ndg. Franscesco Bonanome.
Makamu wa Askofu wa Jimbo Katoliki Shinyanga, Padri Kizito Nyanga akizungumza na viongozi na watendaji mbalimbali katika hafla ya uzinduzi wa jengo jipya la Huduma za tiba na matunzo kwa watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (CTC ) Juni 18, 2020 lililojengwa kwa msaada wa Shirika lisilo la Kiserikali la Doctors With Africa- CUAMM kupitia mradi wa; katika Zahanati ya Old Maswa inayomilikiwa na Kanisa Katoliki.
Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa, Dkt. Khamis Kulemba akizungumza na viongozi na watendaji mbalimbali katika hafla ya uzinduzi wa jengo jipya la Huduma za tiba na matunzo kwa watuwanaoishi na Virusi vya Ukimwi (CTC ) Juni 18, 2020 lililojengwa kwa msaada wa Shirika lisilo la Kiserikali la Doctors With Africa- CUAMM kupitia mradi wa Test and Treat; katika Zahanati ya Old Maswa inayomilikiwa na kanisa Katoliki.
Mratibu wa Mradi wa Test and Treat Shinyanga na Simiyu , Ndg. Franscesco Bonanome akizungumza na viongozi na watendaji mbalimbali katika hafla ya uzinduzi wa jengo jipya la Huduma za tiba na matunzo kwa watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (CTC )Juni 18, 2020 lililojengwa kwa msaada wa Shirika lisilo la Kiserikali la Doctors With Africa- CUAMM kupitia mradi wa Test and Treat; katika Zahanati ya Old Maswa inayomilikiwa na Kanisa Katoliki.
Makamu wa Askofu wa Jimbo Katoliki Shinyanga, Padri Kizito Nyanga (wa pili kulia walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na watendaji mbalimbali katika hafla ya uzinduzi wa jengo jipya la Huduma za tiba na matunzo kwa watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (CTC )Juni 18, 2020 lililojengwa kwa msaada wa Shirika lisilo la Kiserikali la Doctors With Africa- CUAMM kupitia mradi wa Test and Treat; katika Zahanati ya Old Maswa inayomilikiwa na Kanisa Kanisa Katoliki.
Sehemu ya mbele ya jengo jipya la Huduma za tiba na matunzo kwa watu wenye Virusi vya Ukimwi (CTC) Juni 18, 2020 lililojengwa kwa msaada wa Shirika lisilo la Kiserikali la Doctors With Africa- CUAMM kupitia mradi wa Test and Treat; katika Zahanati ya Old Maswa inayomilikiwa na Kanisa Katoliki.
********************************
Na Stella Kalinga, Simiyu RS
Shirika lisilo la kiserikali la Doctors With Africa – CUAMM kupitia Mradi wa Test and Treat limejenga jengo jipya la huduma za tiba na matunzo kwa watu wenye maambukizi ya Virusi vya Ukimwi, kukarabati baadhi ya majengo na kuchimba kisima cha maji katika zahanati ya Old Maswa iliyopo Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa jengo hilo (katika zahanati ya Old Maswa inayomilikiwa na Jimbo Katoliki Shinyanga) Juni 18, 2020 kwa niaba ya Askofu wa Jimbo Katoliki Shinyanga, Liberatus Sangu, Makamu wa Askofu huyo Padri Kizito Nyanga, ameishukuru Doctors with Africa- CUAMM kwa msaada huo na kuahidi kuendelea kushirikiana na Serikali na wadau wote walio tayari kuhudumia watu.
“Tunawashukuru sana CUAMM kwa msaada wa jengo hili, vifaa na ukarabati wa majengo mengine katika zahanati ya Old Maswa; Kanisa lina kiu ya kuwafikia watu kwa huduma siyo maneno na liko tayari kushirikiana na wote wanaotaka kuwahudumia watu,” alisema Padri Nyanga.
Aidha, Padri Kizito ameishukuru serikali kwa kuliamini kanisa hususani jimbo Katoliki Shinyanga, kuliamini kanisa katika kutoa huduma kwa wananchi, kulidhamni katika kuendeleza huduma na kutoa ushauri wa mara kwa mara katika uendeshaji wa taasisi za kanisa.
Akizungumza kwa niaba ya Serikali katika uzinduzi wa jengo hilo Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dkt.Khamis Kulemba amesema CUAMM ni miongoni mwa wadau ambao wanafanya kazi kulingana na malengo ya serikali ya mkoa ya kuboresha miundombinu katika sekta ya afya.
Wakati huo huo Kulemba amewataka wataalam afya katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi kwa kushirikiana na watumishi wa Zahanati ya Old Maswa kuhakikisha huduma zinazotolewa katika jengo hilo la CTC na zahanati hiyo kwa ujumla zinakuwa ni za ubora unaotakiwa na ziendane na thamani ya mradi huo.
Katika hatua nyingine Dkt. Kulemba ametoa wito kwa viongozi wa Dini mkoani Simiyu kuendelea kushirikiana na wataalam wa afya katika kulinda afya ya watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi(VVU), wanaotumia dawa za kufubaza makali ya VVU katika kuwahimiza watumie dawa hizo kwa usahihi badala ya kuwataka kuacha kutumia dawa hizo baada ya kuwaombea.
“Nawaomba viongozi wa dini washirikiane na wataalam kulinda afya za watu wenye VVU, baadhi yao wamekuwa wakiwaombea watu wenye VVU na kuwaambia waache kutumia dawa; watu hao wakiacha kutumia dawa wanakuwa na hali mbaya; kuacha kutumia dawa na kuzirudia tena kunawaletea shida na kutengeneza usugu, nawaomba viongozi wa dini watusaidie kwenye hili,” alisema Kulemba.
Naye Mganga mfawidhi wa zahanati ya Old Maswa Ndaro Lawi amesema huduma za tiba na matunzo kwa watu wenye Virusi vya Ukimwi (VVU) katika zahanati hiyo zilianza mwaka 2016, ambapo hadi sasa jumla ya watu 219 wameandikishwa katika kituo hicho na wanapata huduma mbalimbali bila malipo.
Kwa upande wake Mratibu wa mradi wa Test and Treat kutoka Doctors With Africa- CUAMM mikoa ya Shinyanga na Simiyu, Ndg. Ndg. Franscesco Bonanome amewashukuru viongozi wa Serikali, Jimbo Katoliki Shinyanga na watumishi wa CUAMM, kwa namna walivyofanya kazi kwa ushirikiano na kuahidi kuwa shirika hilo litaendelea kufanya mambo makubwa siku za zijazo.
Ujenzi wa Jengo la CTC na ukarabati wa majengo mengine katika Zahanati ya Old Maswa umegharimu shilingi 209, 885, 665/= huku uchimbaji wa kisima ukigharimu shilingi 39,533,540/=