Home Siasa NDUGU NGEMELA LUBINGA AKUTANA NA VIONGOZI WA CHAMA NA SERIKALI MKOANI GEITA.

NDUGU NGEMELA LUBINGA AKUTANA NA VIONGOZI WA CHAMA NA SERIKALI MKOANI GEITA.

0
…………………………………………………………………………………
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (Siasa na Uhusiano wa Kimataifa) na Mjumbe wa Kamati Kuu CCM ambaye pia ni Mlezi wa Mkoa Geita amekutana na kuzunguza na Viongozi wa CCM Mkoa, Katibu Tawala Mkoa, Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri na Mji Geita.

Katika mazungumzo hayo Ndugu Lubinga amepongeza Viongozi hao kwa kupata dhamana ya kufanya kazi na kuwa Viongozi Mkoani hapo kwani dhamana waliyonayo ni kubwa hivyo kila mtu kwenye nafasi yake ahakikishe anatimiza wajibu wake.

Mlezi huyo wa Mkoa wa Geita amewapongeza sana Viongozi hao jinsi wanavyoendelea kuchukua tahadhari ya Ugonjwa wa CORONA na kumpongeza Rais John Pombe Joseph Magufuli jinsi alivyoweza kupamba na janga hilo na kufanikiwa kwa kiasi kikubwa sana kututoa hofu Watanzania.

Pia ameupongeza Uongozi wa CCM wa Mkoa na Serikali kwa kuleta maendeleo ya haraka kwa muda mfupi kwani rasilimali zote hizo zilikuwepo muda wote lakini maendeleo yalikuwa kidogo sana.

Amewasisitiza viongozi hao kuendelea kuwahudumia wananchi kwa kuwatendea haki maana CCM haikubaliani na Uovu na kuwataka wote kwa pamoja kupambania Chama Cha Mapinduzi kuhakikisha uchaguzi ujao kinashinda kwa kishindo.

Akitoa shukurani zake kwa Mlezi huyo Mkuu wa Mkoa wa Geita Mheshimiwa Eng.Robert Gabriel amesema Geita ni eneo ambalo sasa hivi linavutia kuishi na anawakaribisha Watanzania wote kwenda kuishi na kuwekeza Mkoani humo.

Imeandaliwa na;
IDARA YA SIASA NA UHUSIANO WA KIMATAIFA (SUKI).