Katika mazungumzo hayo Ndugu Lubinga amepongeza Viongozi hao kwa kupata dhamana ya kufanya kazi na kuwa Viongozi Mkoani hapo kwani dhamana waliyonayo ni kubwa hivyo kila mtu kwenye nafasi yake ahakikishe anatimiza wajibu wake.
Mlezi huyo wa Mkoa wa Geita amewapongeza sana Viongozi hao jinsi wanavyoendelea kuchukua tahadhari ya Ugonjwa wa CORONA na kumpongeza Rais John Pombe Joseph Magufuli jinsi alivyoweza kupamba na janga hilo na kufanikiwa kwa kiasi kikubwa sana kututoa hofu Watanzania.
Amewasisitiza viongozi hao kuendelea kuwahudumia wananchi kwa kuwatendea haki maana CCM haikubaliani na Uovu na kuwataka wote kwa pamoja kupambania Chama Cha Mapinduzi kuhakikisha uchaguzi ujao kinashinda kwa kishindo.
Akitoa shukurani zake kwa Mlezi huyo Mkuu wa Mkoa wa Geita Mheshimiwa Eng.Robert Gabriel amesema Geita ni eneo ambalo sasa hivi linavutia kuishi na anawakaribisha Watanzania wote kwenda kuishi na kuwekeza Mkoani humo.
Imeandaliwa na;
IDARA YA SIASA NA UHUSIANO WA KIMATAIFA (SUKI).