Mshambuliaji wa Manchester City, Raheem Sterling akikimbia kushangilia baada ya kufunga bao la kwanza dakika ya 45 na ushei kabla ya Kevin De Bruyne kufunga la pili dakika ya 51 kwa penalti na Phil Foden kufunga la tatu dakika ya 90 na ushei katika ushindi wa 3-0 dhidi ya Arsenal usiku wa Jumatano Uwanja wa Etihad Jijini Manchester.