Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw. Gerald Kusaya,akimsikiliza Mratibu wa Mradi wa Sumukuvu Bw.Clepin Mbekomize wakati akitoa wasilisho kwa wajumbe waliohidhuria warsha hiyo ya kusaini iliyofanyika jijini Dodoma.
Mratibu wa Mradi wa Sumukuvu Bw.Clepin Mbekomize akitoa semina kwa waliohidhuria warsha hiyo ya kusaini iliyofanyika jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw. Gerald Kusaya,akizungumza na wadau kabla ya kusaini Mkataba wa mashirikiano na SIDO iliyofanyika jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa SIDO Mhandisi. Prof. Sylvester Mpanduji,akizungumza na wadau kabla ya kusaini Mkataba wa mashirikiano na Wizara ya Kilimo hafla hiyo imefanyika jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw. Gerald Kusaya,akiteta jambo naMkurugenzi wa SIDO Mhandisi. Prof. Sylvester Mpanduji kabla ya kusaini Mkataba hafla iliyofanyika jijini Dodoma.
Sehemu ya wajumbe waliohudhuria warsha ya kusainiwa mkataba baina ya wizara ya Kilimo na SIDO iliyofanyika jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw. Gerald Kusaya,akiwa na Mkurugenzi wa SIDO Mhandisi. Prof. Sylvester Mpanduji wakisaini mkataba wa mashirikiano hafla iliyofanyika jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw. Gerald Kusaya,akibadilisha mkataba na Mkurugenzi wa SIDO Mhandasi Prof.Sylvester Mpanduji mara baada ya kusaini mkataba huo tukio hilo limefanyika jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw. Gerald Kusaya,akiwa na Mkurugenzi wa SIDO Mhandisi Prof.Sylvester Mpanduji wakionyesha mikataba kwa wajumbe (hawapo pichani) mara baada ya kuingia mkataba wa mashirikiano hafla iliyofanyika jijini Dodoma
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw. Gerald Kusaya,akipeana mkono na Mkurugenzi wa SIDO Mhandisi Prof.Sylvester Mpanduji baada ya kuingia mkataba wa mashirikiano tukio hilo limefanyika jijini Dodoma.
………………………………………………………………………………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
Katika kuhakikisha tatizo la sumukuvu linapungua hapa nchini, Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw. Gerald Kusaya amesaini mkataba wa ujenzi wa vihenge baina ya Wizara ya Kilimo na Shirika la kuhudumia viwanda vidogo vidogo (SIDO).
Katibu Kusaya amesema kuwa lengo la warsha hiyo ni kusaini mikataba miwili ambayo inahusiana na mradi wa Sumukuvu katika kuimarisha usalama wa chakula na kusaidia kutengeneza vihenge. Hata hivyo Kusaya amesema mradi wa sumukuvu umetokana na kutohifadhi vizuri chakula hasa katika mazao ya karanga na mahindi.
Aidha, Bw.Kusay amesema kuwa Serikali imetoa kiasi cha shilingi Bilioni 3.8 ambazo zitapelekwa SIDO ili ziweze kusaidia kutoa mafunzo ya vihenge.
Kusaya amesema atazifuatilia fedha hizo ili kuona zinatumika vizuri na kuwataka watendaji wakuu wa SIDO kutimiza wajibu wao katika suala hili. Na amewasisitizia wananchi juu ya upendo alionao Mhe. Rais Magufuli kwa kuwapatia mradi huu ambao utasaidia kutokomeza tatizo hili.
“ Hizi fedha sio zetu ni fedha za umma, za walipa kodi” amesisitiza Kusaya
Hata hivyo Kusaya ametoa wito kwa wananchi kuwa miradi itakapokamilika waitunze ili iwasaidie kwani tatizo hili la sumukuvu ni kubwa. Aidha,katika kutekeleza mradi huu Kusaya amesema Wizara itashirikiana na taasisi nyingi kama SIDO, VETA, TPRI, TARI, CPB, TBS na taasisi nyingine ambazo zinahusiana na masuala ya chakula.
“ Ni jukumu letu sisi Wizara kuhakikisha hii mipango tunayopanga inakamilika kwa wakati na sisi Wizara ya Kilimo hatuwezi kutekeleza peke yetu ndio maana tunashirikiana na wananchi” amesema Kusaya
AidhaKusaya amesema kuwa baada ya siku chache Wizara itasaini tena mkataba na wakandarasi ambao wataenda kujenga maabara na Kituo mahiri cha Usimamizi wa mazao ya nafaka.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa SIDO Mhandisi. Profesa. Sylvester Mpanduji amesema kuwa Kiwanda hicho kitashiriki katika kutoa teknolojia, mafunzo, mikopo na kuhamasisha kutafuta masoko ili viwanda vidogo vipate wanunuzi.
Naye Mratibu wa Mradi wa Sumukuvu Bw. Clepin Mbekomize amesema kuwa VETA inatarajia kutoa mafunzo kwa vijana 400 ambapo watapata mafunzo ya teknolojia ya kutengeneza vihenge na itawasaidia katika kuwapatia ajira vijana hao