Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge) Bw. Tixon Nzunda pamoja na timu aliyoongozana nayo wakiwa katika ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la ofisi ya Tume ya Uchaguzi (NEC) lililopo eneo la Njedengwa Jijini Dodoma.
Mhandisi wa mifumo ya zima moto, Gaudence Kessy akitoa ufafanuzi wa masuala ya ufungaji wa mifumo hiyo wakati wa kikao cha majumuisho mara baada ya ziara ya Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge) Bw. Tixon Nzunda.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge) Bw. Tixon Nzunda akitoa majumuisho ya ziara yake katika Jengo la NEC kwa timu inayosimamia ujenzi huo.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge) Bw. Tixon Nzunda akitoa maelekezo kwa wasimamizi wa mradi wa ujenzi wa jengo la ofisi ya Tume ya Uchaguzi (NEC) alipotembelea kukagua maendeleo ya mradi huo Juni 18, 2020.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge) Bw. Tixon Nzunda akitoa maelekezo kwa Msimamizi na Meneja wa Mradi wa Ujenzi kutoka Chuo kikuu cha Ardhi, Godwin Maro wakati alipotembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la Ofisi za Tume ya Taifa ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) lililopo eneo la Njedengwa Dodoma Juni 18, 2020 unaosimamiwa na Kikosi cha SUMA JKT.
Msimamizi na Meneja wa Mradi wa Ujenzi kutoka Chuo kikuu cha Ardhi, Godwin Maro akimuonesha maendeleo ya ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge) Bw. Tixon Nzunda wakati wa ziara yake ya kukagua ujenzi wa ofisi hizo zilizopo eneo la Njedengwa Jijini Dodoma Juni 18, 2020.
Mhandisi wa mifumo ya zima moto, Gaudence Kessy akitoa ufafanuzi wa hatua za ufungaji wa mifumo hiyo kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge) Bw. Tixon Nzunda wakati wa ziara hiyo.
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)