Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mhe. Anthony Mavunde akikabidhi mifuko ya cement kwa ajili ya ujenzi wa shule ya sekondari katika kata ya Maoma Makulu iliyopo jijini hapo.
Baadhi ya wananchi wakishusha mifuko ya cement iliyotolewa na Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mhe. Anthony Mavunde kwa ajili ya ujenzi wa shule ya sekondari katika kata ya Mahoma Makulu iliyopo jijini hapo.
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mhe. Anthony Mavunde akiwa na wananchi wa kijiji cha Mahoma Makulu Kata ya Chahwa wakiwa katika shughuli za ujenzi wa shule ya sekondari katika kata ya Maoma Makulu iliyopo jijini hapo.
……………………………………………………………………………..
Na.Majid Abdulkarim, Dodoma
Wananchi wa kijiji cha Mahoma Makulu Kata ya Chahwa kwa kushirikiana na Mbunge wao wa Jimbo la Dodoma Mjini Mhe. Anthony Mavunde wajifunga kibwebwe kujenga shule ya sekondari katika kata hiyo ili kutatua changamoto ya Watoto wao kutembea mwendo mrefu wa zaidi ya kilometa kumi kutafuta elimu.
Hayo yamebainishwa leo jijini Dodoma katika uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa shule ya sekondari katika kata ya Mahoma Makulu.
Aidha Mhe. Mavunde amesema kuwa ili kuweka alama ya kutatua changamoto ya Watoto wa kata hiyo kutembea mwendo mrefu kutafuta elimu lazima washirikiane katika kila hatua ya ujenzi wa shule hiyo ili ifikapo januari 20212 watoto hao waanze kidato cha kwanza katika shule hiyo.
“Mimi jukumu langu ni kuchochea maendeleo kwenu nyinyi hivyo tushirikiane kama tulivyo anza leo katika uchimbaji wa msingi ili kufikia malengo ya kutatua changamoto hii katika kata yetu”, amesema Mhe. Mavunde.
Hivyo Mhe. Mavunde ametoa wito kwa wananchi hao kukamilisha ujenzi wa msingi ndani ya siku chache na mafundi kutanguliza uzalendo katika kufanyikisha ujenzi huo kwa wakati ili Watoto waweze kupata huduma bora ya elimu ndani ya maeneo yao.
Katika hatua nyingine Mhe. Mavunde amekuta wananchi wa kata hiyo washakamilisha upatikanaji wa tofali 900 na baadhi ya mifuko ya saruji hivyo nayeye kama kiongozi ameunga mkono juhudi hizo kwa kuchangia tofari 5,000, mifuko ya saruji 100,kokoto na mchanaga ili kuongeza chachu katika kukamilisha ujenzi huo kwa wakati.
Mhe. Mavunde ametoa rai kwa wananchi hao kuimarisha ushirikiano katika kukamilisha ujenzi huo na kutanguliza uzalendo ili kuweka alama katika maendeleo ya kata hiyo.