………………………………………………………………………………..
Mlezi wa Mkoa wa Geita Ndugu. Ngemela Lubinga ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM (Siasa na Uhusiano wa Kimataifa) amefanya ziara wilayani Chato na Mbogwe Mkoani Geita.
Wilayani Chato Ndugu Lubinga amekagua na kujionea upanuzi wa Hospital ya Wilaya ya Chato pamoja na maendeleo ya mradi wa ujenzi wa majengo matano ambao umekamilika kwa asilimia 97%.
Aidha amekagua pia maendeleo ya ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Mlimani ambao umejengwa kwa nguvu ya Wananchi kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Chato, Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo la Chato,Mkuu wa Mkoa Geita, Mkuu wa Wilaya Chato na Diwani wa kata ya Muungano.
Ndugu Lubinga pia akiwa Wilayani Chato ametembelea na kukagua ujenzi wa ofisi ya Chama Cha Mapinduzi Tawi la Bomani kata ya Muungano ambapo wananchi hao na viongozi wa Tawi wamemshukuru Mkuu wa Mkoa Geita *Mhe.Eng Robert Gabriel* kwa kuwanunulia kiwanja hicho.
Pamoja na ukaguzi huo Ndugu Lubinga amewataka Viongozi na wanachama wa CCM Wilayani Chato kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili kuendelea kumpa heshma Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania *Dkt John Pombe Joseph Magufuli* ambaye anatokea Wilayani CHATO.
Akiwa Wilayani Chato Ndugu Lubinga amesema ‘’Rais Magufuli ndio mtu pekee anayeweza kushughulika na matatizo ya Nchi na ya Watanzania wote tumeshuhudia kwenye janga la CORONA “ amewasisitiza viongozi wote kuwa wanapopewa madaraka waangalie matakwa ya mfumo na kutakiwa kuwa wanyenyekevu.
Wilayani Mbogwe, Mlezi huyo wa Mkoa wa Geita alikagua Ujenzi wa mradi wa vyumba 10 vya madarasa, bwalo la chakula, na mabweni mawili ya shule ya Sekondari Nyakasaluma.
Pamoja na hayo pia alipokea taarifa ya hali ya Kisiasa Wilaya ua Mbogwe na kukagua Ujenzi wa vyumba 22 vya madarasa katika shule ya msingi Kasandalala.