Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Benki ya NMB, Juma Kimori (aliyenyoosha mkono) akimwelezea jambo Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Jenerali, Charles Mbuge ( wapili kushoto) wakati wafanyakazi wa benki hiyo, walipotembelea Makao Makuu ya Jeshi hilo Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma.
Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Benki ya NMB, Juma Kimori (wa kwanza kushoto) akimpongeza Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Jenerali, Charles Mbuge (katikati) kwa kupandishwa cheo kuwa Mkuu wa JKT, wakati wafanyakazi wa benki hiyo, walipotembelea Makao Makuu ya Jeshi hilo Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma. Kulia ni Meneja Mahusiano na Serikali wa Benki ya NMB, Josephine Kulwa na Meneja wa Kanda ya Kati, Nsolo Mlozi (wapili kulia).