NA MWL FREDERICK J NDAHANI –SINGIDA
[email protected] -0757622794
************************************
MH John Pombe Joseph Magufuli alizaliwa Oktoba 29,mwaka 1959 katika kijiji cha Chato,wilayani Biharamuro katika Mkoa wa Kagera .hivi sasa Chato ni Wilaya katika Mkoa wa Geita.
Mh Magufuli ni Daktari wa Falsafa (PhD) ya Kemia .Amejaliwa Mke na watoto Saba.Mh Magufuli alichaguliwa na Watanzania kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwezi Oktoba ,2015 kwa tiketi ya CCM na kuapishwa ili aanze majukumu yake rasmi ya kuingoza Tanzania tarehe 5 Novemba ,2015 .Aidha alifungua bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 20 Novemba 2015.
Rais anapolivunja Bunge la 11 leo tarehe 16 June 2020,Rais Magufuli ameonesha kuwa ana sifa zote muhimu za uongozi ,Ana Dira ,maono na malengo ya kulijenga Taifa letu kule anakotaka liwe na kuwaletea maendeleo makubwa Watanzania.
Rais haogopi kufanya maamuzi makini katika Nyanja mbalimbali na hata pale tulipo kuwa katika kipindi cha ugonjwa wa COVID 19 aliwahimiza watanzania kumutanguliza Mungu wakati wote na leo hii tunashuhudia kupungua kwa ugojwa wa corona na shughuli mbalimbali kurejea kama kawaida na Rais ametangaza kufunguliwa kwa shule za awali,msingi na sekondari tarehe 29 June 2020 .
Ana kiu ya kuona Taifa linapata maendeleo .Amejipambanua kuwa mtetezi wa wanyonge na dhamira yake kubwa ni kuona Wananchi wanapata huduma bora za jamii na kero zao zinaondoka katika nyanja mbalimbali.Sisi kama watanzania ni mashuhuda wa mafanikio haya katika sekta za elimu,afya,kilimo,biashara,umeme,maji,usafiri na usafirishaji,mifigo.uvuvi,utawala bora,ukasanyaji na usimamizi wa mapato na michezo pamoja na utamaduni.
Rais Dkt Magufuli alianza elimu ya Msingi katika shule ya Msingi Chato mwaka 1967 na kumaliza mwaka 1974.Mwaka 1975 alianza masomo ya sekondari katika shule ya Seminari ya Katoke Mkoani Kagera na kuhamia shule ya Sekondari Lake iliyopo Mwanza mwaka 1977.alihitimu kidato cha nne mwaka 1978.mwaka 1979 na 1981 alifanya masomo ya kidato cha Tano na Sita katika shule ya Sekondari ya Mkwawa Mkoa wa Iringa.
Aidha 1981 hadi 1982 alisoma Chuo cha Ualimu Mkwawa na kuhitimu Stashahada ya Ualimu ya Masomo ya Kemia ma Hisabati,yeye ni Mwalimu kweli kweli.Mwezi Julai hadi Disemba mwaka 1983 Rais Magufuli alipata mafunzo ya kijeshi katika Jeshi la Kujenga Taifa kikosi cha Makutupora Mkoa Dodoma,baadaye alihamishiwa kikosi cha mafunzo ya kujenga Taifa Makuyuni –Arusha Machi 1984 na alimaliza mafunzo june mwaka 1984 baada ya kuhamishiwa Mpwapwa Dodoma.
Mwaka 1985 Rais Magufuli alijiunga na chuo kikuu cha Dar es Salaam kusoma Shahada ya kwanza ya Sayansi nna Ualimu akijikita katika Masomo ya Kemia na Hisabati .Mh Rais alitunukiwa Shahada hiyo mwaka 1988.Mwaka 1991 hadi 1994 alisoma na kutunukiwa Shahada ya Uzamili katika fani ya Kemia iliyotolewa na chuo kikuu cha Dar es Salaam na Chuo kikuu cha Salford cha Uingereza.
Mwaka 2006 alijiunga na chuo Kikuu cha Dar es salaam kwa ajili ya Shahada ya Uzamivu katika fani ya Kemia na kufanikiwa kuhitimu mwaka 2009.
UZOOEFU WA NDANI YA SERIKALI
Rais Magufuli alikuwa mwalimu katika shule ya sekondari Sengerema iliyopo Mkoani Mwanza akifundisha Masomo ya Kemia na Hisabati na baadae kujiunga na Chama cha Ushirika cha Nyanza Mkoani Mwanza akiwa Mkemia Mkuu hadi mwaka 1995.
Mwaka 1995 alichaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Biharamulo Mashariki Mkoani Kagera.Aidha Rais wa Awamu ya Tatu Mheshimiwa Benjamini W Mkapa alimuteuwa kuwa Naibu waziri wa Ujenzi aliitumikia hadi Mwaka 2000.Mwaka 2000 alichaguliwa kuwa Mbunge tena bila kupigwa katika jimbo la Biharamulo Mashariki na kuteuliwa kuwa waziri kamili wa ujenzi hadi mwaka 2005.
Mwaka 2005 Rais Magufuli alichaguliwa tena bila kupingwa katika jimbo lake na Rais wa Awamu ya Nne Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete alimuteuwa kuwa Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuanzia mwaka 2005 hadi 2008 ambapo alihamishiwa Wizara ya Mifugo na maendeleo ya Uvuvi hadi mwaka 2010.
Baada ya mgawanyo wa majimbo Rais Magufuli alichaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Chato na kuteuliwa kuwa Waziri wa ujenzi mwaka 2010 hadi 2015.
Rais Magufuli alishiriki katika Bunge maalumu la kutunga katiba Mpya akiwa mjumbe Mwaka 2014.Akiwa waziri wa Aridhi ,Nyumba na Maendeleo ya Makazi aliweza kuwachaguliwa kuwa Mwenyekiti mweza (Co-Chair) wa Mkutano wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Makazi (UN-Habitat).
Rais John Joseph Magufuli alichaguliwa na wananchi wakiwa na matumaini makubwa kwake 25 Oktoba ,2015 kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuapishwa kushika rasmi wadhifa huo tarehe 5 Novemba ,2015.
Dkt Magufuli ni kiongozi mnyenyekevu aliye na hofu ya Mungu,mkweli,mtekelezaji wa ahadi ,mwadilifu,shupavu,mahiri,mbunifu,mtafiti,mchapakazi na mtetezi wa wanyonge.Ni kiongozi mpenda haki na mchukia dhuluma ,Rushwa ,ufisadi na ubaguzi wa aina yoyote ile.Ni kiongozi mwenye msimamo na mtetezi wa yale anayoaamini.
Katika Urais wa awamu ya miaka mitano amefanya kazi kwa uadilifu na umahiri mkubwa ,amejipambanua kuwa mfuatiliji na msimamizi wa sheria.Magufuli anasifika sana kwa uwezo wake wa kutunza kumbukumbu ya kazi zake na leo alipo lihutubia Bunge na kulivunja tumejionea anapotaja mafanikio ya serikali yake ya Awamu ya Tano ametaja barabara kwa takwimu na maeneo ambayo ametekeleza miradi mabalimbali ya maendeleo.
Rais Magufuli ametekeleza ahadi zake alizozitoa kwa asilimia kubwa na nikiwa Mwalimu nampatia Daraja la A .
Wakati akizindua Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 20 Novemba 2015,Rais Dtk.Magufuli alitaja malengo mahususi ya Serikali ya Awamu ya Tano .Malengo hayo ni kama ifuatavyo:-
1.Kudumisha Muungano ,Amani na Umoja wa Tanzania ,Seriali haitamuonea aibu mtu mwenye nia ya kuvunja Muungano na kuvuruga Amani na mshikamano wa Nchi .Hili limejidhirisha vizuri wakati wa uchaguzi wa marudio huko Zanzibar kwani uchaguzi ulifanyika kwa Amani na utulivu.
2.Kujenga uchumi wa viwanda ili kufikia azma ya kuwa nchi ya uchumi wa kati kulingana na malengo ya Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025.viwanda vingi zimeendelezwa na kujengwa ambapo umesaidia kupunguza tatizo la ajira na umaskini pamoja na kukuza pato la Taifa na Uchumi .
3.Kuongeza kasi ya ujenzi wa miondombinu ya kiuchumi .hususani miondombinu ya usafiri na nishati.Tumejionea Ndege,meli,Barabara,viwanja na reli ya kisasa.
4.Kuimarisha huduma za jamii,hususani Elimu,Afya na Maji .Lengo hili limefanikiwa kwa upatikanaji wa huduma hizo kwa urahisi na ubora unaostahili ili kukabiliana na ujinga ,umaskini na maradhi.
5.Kusimamia uwajibikaji wa utumishi wa umma na kuondoa urasimu wa ndani ya serikali.Lengo limefanikiwa kwani watumishi wa umma wanafanya kazi kwa ueledi,uadilifu na kujituma ili kuwawezesha wananchi kupata huduma bora na kwa wakati.
6.Kuimarisha usimamizi wa rasimali za nchi ikiwemo kuhifadhi mazingira na kuzidisha vita dhidi ya ujangili .lengo limefanikiwa kwa kuwa rasilimali za nchi zinawanufaisha watu wa kizazi cha sasa na kijacho ikiwemo madini na misitu aidha ukusanyaji wa mapato ya serikali na udhibiti wa matumizi ya serikali nao umeimarishwa.
7.Kusimamia utawala bora unaozingatia sheria na haki za Binadamu .Jitihada za makusudi zimetekelezwa katika mapambano dhidi ya Rushwa ,usafidi,dhuruma na uonevu wa aina yoyete.aidha maslahi ya makundi ikiwemo kupatiwa mikopo bila riba vijana,walemavu na wanawake pamoja wazee na watoto maslahi yao yamelindwa.Wananchi tumehimizwa kuheshimu na kufuata sheria za nchi.
8.Kulinda usalama wa raia na mali zao kwa kupambana na uhalifu ,ikiwemo wizi,ujambazi ,tatizo la dawa za kulevya.Watanzania kwa sasa tuna Amani na kushiriki kazi za maendeleo kila kubughudhiwa na uhakika wa usalama wa mali zao umeimarika.
9.Kudumisha na kuendeleza ujirani mwema ,mahusiano mema na mataifa mengine duniani pamoja na mashirika ya kimataifa na kikanda.
10.Kuendeleza na kusimamia vizuri shughuli za michezo ,Sanaa,burudani na utamaduni ikiwemo kukuza lugha ya Kiswahili.
Rais katika hotuba yake ya kufunga Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 16 June 2020 ameleza kinagaubaga mafanikio makubwa yaliyofanyika katika miaka mitano na sisi watanzania tumejiona kwa macho mafanikio haya hatuna budi kuendelea kumwamini tena kwa miaka mitano ijayo hadi 2025.
Hitimisho
Watanzania wote ni wajibu wetu wa kulinda miradi yote na kumuombea Rais wetu mpendwa Dtk.John Pombe Magufuli na wasaidizi wake ili malengo na azma ya serikali ya awamu ya Tano iweze kufanikiwa,Tumpatie nafasi Mheshimiwa Magufuli miaka mitano 2020 hadi 2025 ili Watanzania tuendelee kufaidi matunda ya Rais wetu ambaye ni chagua la Mungu kwetu watanzania .kwani amedhamiria kuongeza kasi ya ukuaji wa maendeleo ya kiuchumi na sisi watanzania kushiriki kufanya kazi kwa bidii na maarifa ndani ya falsafa ya HAPA KAZI TU. Dhamira ya Rais wetu kwa miaka mitano ijayo ni kuwezesha Taifa letu kufikia uchumi wa kati unaoongozwa na viwanda na huduma bora kwa wananchi ili kutimiza malengo ya Dira ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2025.