Wachezaji wa Yanga SC wakiwa Bungeni Jijini Dodoma leo pamoja na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa Michezo, Dk Harrison Mwakyembe na Naibu wake, Juliana Shonza. Kikosi cha Yanga kimetambulishwa leo Bungeni baada ya kuwasili Dodoma kwa ajili ya mchezo wake wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Jumatano dhidi ya JKT Tanzania Uwanja wa Jamhuri
………………………………………………………………………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
Kikosi cha Yanga pamoja viongozi wake wametinga bungeni leo jijini Dodoma na kukaribishwa kwa shwangwe nyingi kutoka kwa wabunge pamoja na Spika wa Bunge,Job Ndugai huku jina la mchezaji,Bernard Morrison likiwa gumzo ndani ya bunge hilo.
Yanga ametinga leo wakiwa katika jiji la Dodoma wakijiandaa na mchezo wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya wenyeji JKT Tanzania mchezo utakaopigwa kesho Jumatano katika uwanja wa Jamhuri Dodoma.
Yanga wanashuka uwanjani wakiwa na morali kubwa baada ya Jumamosi waliweza kupata ushindi ugenini wa bao 1-0 dhidi ya Mwadui ya Shinyanga mchezo uliochezwa katika uwanja wa Kambarage.
Akiitambulisha timu hiyo bungeni,Spika wa Bunge, Job Ndugai alihoji alipo Morrison huku akiwataka Wabunge mashabiki wa timu ya Simba wawashangilie Yanga.
“Waheshimiwa wabunge wanauliza mchezaji mmoja tu sijui Morrson naomba asimame Morrison yupo, yupo eeeeh, hayupo bwana, hayupo hayupo naomba wale Waheshimiwa wa Simba wapeni makofi kidogo.
Morrson anakumbukwa na Mashabiki wa Simba Machi 8 mwaka huu timu yao mbele ya Rais Dkt.Magufuli ,Rais wa CAF pamoja na viongozi mbalimbali Yanga walipoibuka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Bernad Morrison kwa njia ya faulo
“Msisahau tu kwa Yanga ule mkuki mmoja, ule bado tunaukumbuka sana tutakapokutana tena Mjiandae kisawasawa maana itarudi mikuki mingi mno ,”alisisitiza Spika huku bunge likizizima kwa shangwe na makofi