Home Siasa NCCR MAGEUZI WAANZA RASMI KUTOA FOMU ZA UGOMBEA

NCCR MAGEUZI WAANZA RASMI KUTOA FOMU ZA UGOMBEA

0

*****************************

Na Magreth Mbinga

Katibu mkuu wa NCCR MAGEUZI Elizabeth Mhagama amesema wanawakaribisha Watanzania wote ambao walishiriki kwenye mageuzi kushiriki katika kugombea nafasi za uongozi kama wanavigezo.

Amezungumza hayo leo kwenye makoa Makuu ya Chama hiko Ilala Jijini Dar es Salaam.

Pia amesema Mgombea awe na sifa za kiongozi na bora ambazo zimeanishwa na Katiba ya Chama hiko.

Vilevile Mhagama amesema Mgombea huyo lazima asimamie maslahi ya wengi dhidi ya watu wachache.

Sanjari na hayo wametoa ratiba ya uteuzi wa wagombea na mchakato huo unaanza leo Juni 15 hadi July 8 kwa ngazi ya Urais,Ubunge,Udiwani,wawakilishi TZ na ZNZ.