******************************
Kamati ya utekelezaji ya Baraza la Umoja wa wanawake wa Tanzania wilaya ya Dodoma Mjini,
wamuunga mkono Rais Dkt.John Pombe Joseph Magufuli katika sekta ya elimu na afya.
Kamati hiyo imefika katika kituo Cha afya Cha Mkonze Jijini Dodoma ambapo wamekabidhi Mashuka kwa ajili ya wagonjwa wote watakaohudumiwa katika kituo hicho.
Sanjari na hayo,wametoa vifaa vya kuandikia kwa wanafunzi wote wa kidato Cha sita(watahiniwa) katika shule ya sekondari (upili) ya wasichana Msalato
Vifaa vilivyotolewa ni kalamu za wino boksi 20, Mathemacal sets 244,Rula 60,kalamu za risasi 244, vifutio na vichongeo.
Mwenyekiti wa UWT wilaya ndugu Winifrida Aloyce Kaliyo amewahimiza wanafunzi wafanye vizuri katika mitihani yao ya kuhitimu.
Katibu wa UWT wilaya amewakumbusha wanafunzi kuwa wazalendo wa taifa hili kwani wao ndio viongozi na watumishi wa serikali wajao.
Pia mwakilishi wa afisa elimu sekondari jiji la Dodoma ndugu Malale amewashukuru sana UWT wilaya hii na kuwaomba waendelee na moyo huo kuipa nguvu sekta ya elimu.