**********************************
Na John Walter-Babati
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Babati Hamisi Iddi Malinga amefariki dunia asubuhi ya leo June 14,2020.
Akithibitisha kutokea kwa kifo hicho Mkuu wa wilaya ya Babati Elizabeth Kitundu amesema mkurugenzi Malinga amefariki wakati akiendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Manyara alipokuwa amelazwa takribani wiki mbili.
Kitundu amesema wilaya ya Babati imepokea kwa masitiko taarifa za msiba huo na kwamba wanashirikiana na familia kufanya taratibu za kusafirisha mwili kwenda Iringa kwa ajili ya Mazishi.
Hamisi Iddi Malinga alikuwa mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya babati kuanzia mwaka 2016 hadi mwaka 2020 umauti ulipomfika.