Home Siasa MWENYEKITI CHASO-UDSM AOMBA VYOMBO VYA USALAMA NCHI KUWEZA KUFANYA UTAFITI

MWENYEKITI CHASO-UDSM AOMBA VYOMBO VYA USALAMA NCHI KUWEZA KUFANYA UTAFITI

0

**********************

Na Magreth Mbinga

Mwenyekiti wa Chadema Student Organisation UDSM (CHASO-UDSM Masoud Mambo ameomba vyombo vya usalama wa nchi kuweza kufanya utafiti juu ya tukio lililomkuta mwenyekiti wa CHADEMA ND Freeman Mbowe.

Hayo ameyazungumza kwenye ofisi ya CHADEMA Kanda ya Pwani na kutaka Mamlaka husika kuweka nguvu kubwa katika hilo.

Pia amesema wao kama vijana watahakikisha wanalinda chama Chao kuelekea uchagizi mkuu.

Vilevile ameishauri tume ya uchaguzi kuandaa namna ya mfumo wa wanafunzi kushiriki katika kupiga kura pindi watokapo mashuleni .

“Tume ya Taifa irekebishe mfumo ambao wanatumia sababu wanafunzi wanapojiandikisha wanakuwa bado wapo mashuleni na uchaguzi unawakuta wapo nyumbani mtu huyu ananyimwa haki yake ya kuchagua kiongozi anaemtaka”amesema Mambo.