Home Mchanganyiko RC.MAKONDA AMEWATAKA VIJANA WA CCM (UVCCM) DAR KUJITAHADHARI

RC.MAKONDA AMEWATAKA VIJANA WA CCM (UVCCM) DAR KUJITAHADHARI

0

********************************

Na Magreth Mbinga

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh Paul Makonda amewataka vijana wa CCM (UVCCM) Mkoani humo wawe macho na watu ambao wanania ya kuhatarisha amani ya uchumi wa Taifa.

Hayo ameyazungumza Leo katika mkutano wa UVCCM katika ukumbi wa Anatogo uliopo Mnazi mmoja Jijini Dar es Salaam.

Pia amesema kitendo Cha Mh Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Magufuli kujenga mradi wa umeme kupitia bwawa la Mwl Nyerere umeumiza watu wengi Sana hasa wale wasiopenda maendeleo ya nchi.

Vilevile Rc Makonda amewataka vijana hao wachague viongozi bika kujali muonekano,cheo au ukaribu wa mtu huyo bali waangalie vigezo vya mgombea ili kupata viongozi makini na waadilifu.

Sanjari na hayo Rc Makonda amewataka vijana wa Mkoa wa Dar es Salaam wasiwe moja ya watu wanaosubiri posho ili kukisemea chama.

“Naomba vijana wote tunapoanza ziara za kukabidhi miradi kila Wilaya mujitokeze kwa wingi “amesema Rc Makonda.

Hata hivyo Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mh Mrisho Gambo amewatia moyo vijana na kuwataka waendelee kushirikiana,kupeana moyo na fursa ili kuweza kupata viongozi bora.

“Mkahakikishe kiak Wilaya mnayasema yale yote ambayo Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ameyafanya sababu yapo na yanaonekana.