Mwenyekiti wa halmashauri ya Arusha DC Baraka Simon akizungumza katika kikao Cha kuvunja Baraza la madiwani katika halmashauri ya Arusha (Happy Lazaro)
Madiwani wa halmashauri ya Arusha DC wakiwa katika kikao.cha kuvunja Baraza hilo(Happy Lazaro).
Madiwani wakiwa katika kikao Cha pamoja Cha kuvunja Baraza katika halmashauri ya Arusha DC,(Happy Lazaro).
*************************************
Happy Lazaro,Arusha.
Arusha.Baraza la madiwani halmashauri ya Arusha limeishauri halmashauri hiyo kuwakabithi vyanzo mbalimbali vya mapato mamlaka ya mji mdogo wa Ngaramtoni ili iweze kujiendesha kupitia vyanzo vyake .
Wakizungumza katika Baraza hilo la madiwani ,Diwani wa kata ya Oltoroto ambaye pia ni Mwenyekiti wa halmashauri hiyo ,Baraka Simon alisema kuwa, mamlaka hiyo imeundwa kisheria na inatekeleza majukumu yake ipasavyo ila changamoto kubwa ipo katika fedha za kuiendesha mamlaka hiyo.
Baraka alisema kuwa,kwa pamoja wameliachia jukumu hilo halmashauri hiyo ili waweze kufanya tathmini na kuwapatia vyanzo mbalimbali vya mapato walivyoomba kupewa ili waweze kuviendesha wenyewe na kuweza kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili.
“Tumemwachia mkurugenzi na timu yake kukaa pamoja na kufanya tathmini ya vyanzo hivyo wanavyohitaji ili waweze kupatiwa na hatimaye kuweza kujiendesha wenyewe kuliko fedha zote wanazokusanya ziletwe halmashauri halafu ndo wagawiwe kidogokidogo.”alisema Baraka.
Alifafanua kuwa ,mamlaka hiyo iliomba bajeti ya kiasi Cha shs 137 milioni lakini wamepewa kiasi Cha shs 6 milioni fedha ambazo hazitoshelezi kulingana na mahitaji mbalimbali yaliyopo katika mamlaka hiyo.
Hata hivyo Mwenyekiti huyo alimwelekeza mkurugenzi wa halmashauri hiyo pamoja na mwanasheria kufuatilia na kuchunguza uhalali wa madeni ya zaidi ya shs 49 milioni wanazodai wenyeviti wa vitongoji ambao wanaunda mamlaka ya mji mdogo wa Ngaramtoni ambao ukomo wao uliishia mwaka 2019 ili waweze kulipwa haki zao kwani walifanya kazi kubwa sana.
“Mimi napenda kuwahakikishia madiwani na wananchi kuwa mamlaka ipo hai na haitavunjwa na itaendelea kubaki hai kwani ni chombo ambacho kimeundwa kisheria.”alisema .
Akizungumza kwa upande wa mapato ya halmashauri, Baraka alisema kuwa desemba waliyumba kidogo kutokana na mambo kuwa mengi na kuwafanya kufikia asilimia 35 ya mapato lakini hadi kufikia leo wameweza kufikia asilimia 70 ya mapato kwa maana ya makusanyo ya ndani hivyo wanazidi kupanda siku hadi siku.
“Baraza kwa pamoja tumeweza kuacha maelekezo kwa halmashauri kuwa kufikia June 30 mwaka huu mapato yawe asilimia 80 na inawezekana kutokana na vyanzo mbalimbali vya mapato.”alisema.
Naye Diwani viti maalumu tarafa ya Muna Twalibu alisema kuwa,mamlaka ya mji mdogo wa Ngaramtoni ilianzishwa kisheria kabisa, changamoto kubwa iliyopo ni fedha zinazokusanywa na kuletwa halmashauri kutorudi kwa wakati na ni kiasi kidogo sana.
Alisema kuwa,mamlaka hiyo inapata changamoto kwa ajili ya kuwalipa watendaji wa vijiji ,kodi mbalimbali wanazodaiwa ,wazabuni mbalimbali na wenyeviti wa vijiji,hivyo endapo wakipewa vyanzo vya mapato walivyoomba wataweza kujiendesha wenyewe na kuondokana na changamoto mbalimbali.
“Changamoto ni kwamba fedha zile za vyanzo mbalimbali tunazoleta halmashauri hazirudishwi kwa wakati na zinazorudi ni kidogo hazitoshelezi chochote ,hivyo tunaomba Sana fedha hizo wanazoomba halmashauri iwapatie ili zikafanye kazi mbalimbali kwani kama huna fedha huwezi kujiendesha .”alisema Muna.