Afisa Maendeleo ya Jmaii kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bw. Juma Samuel akifafanua masuala mbalimbali kuhusu haki za Mtoto kwa wawakilishi wa watoto kutoka wilaya za Nyamagana na Ilemela mkoani Mwanza kuelekea Siku ya Mtoto wa Afrika.
Afisa Maendeleo ya Jmaii kutoka Wuzara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bi. Mwelinde Kato akifafanua masuala mbalimbali kuhusu haki za Mtoto kwa wawakilishi wa watoto kutoka wilaya za Nyamagana na Ilemela mkoani Mwanza kuelekea Siku ya Mtoto wa Afrika.
Mwenyekiti wa Baraza la watoto Wilaya ya Nyamagana Mkoa wa Mwanza Godlisten Irunde akichangia mada katika mafunzo kuhusu haki za mtoto kuelekea Siku ya Mtoto wa Afrika.
Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Watoto Tanzania Aidath Ishulula akichangia mada katika mafunzo kuhusu haki za mtoto kuelekea Siku ya Mtoto wa Afrika.
Mjumbe wa Baraza la Watoto mkoa wa Mwanza Samwel Lubilo akichangia mada katika mafunzo kuhusu haki za mtoto kuelekea Siku ya Mtoto wa Afrika.
Mjumbe Kamati Kuu Baraza la Watoto Taifa Apwiyamwene Mchopa akichangia mada katika mafunzo kuhusu haki za mtoto kuelekea Siku ya Mtoto wa Afrika.
Baadhi ya wawakilishi wa watoto kutoka katika Wilaya za Ilemel na Myamagana mkoani Mwanza wakifuatilia mafunzo na majadiliano yaliyokuwa yakitolewa na Maafisa kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii) kwa kushirikiana na Shirika la Plan International Tanzania kuelekea Siku ya Mtoto wa Afrika.
Picha Zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW
…………………………………………………………………………………
Na Mwandishi Wetu Mwanza
Mwenyekiti wa Baraza la Watoto Wilaya ya Nyamagana Mkoani wa Mwanza Godlisten Irunde ameviomba vyombo vya habari nchini kutoa nafasi watoto kutumia vyombo hivyo kujieleza katika masuala mbalimbali ilikujenga watoto wenye kujiamini katika kuwa taifa imara.
Hayo yamebainishwa hayo katika leo 12/06/2020 mkoani Mwanza katika mafunzo maalum yaliyoandaliwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii) kwa kushirikiana na Shirika la Plan International Tanzania katika kuelekea Siku ya Mtoto wa Afrika kwa mwaka 2020.
Amesema watoto wakishiriki kubainisha na kuzungumzia haki zao watapata ujasiri na kujengewa hali ya kujiamini na kujengeka kisaikolojia katika kung’amua changamoto zinazowakabili na kuweza kuzipatia utatuzi ulio sahihi.
Aidha akizungumza katika mafunzo hayo Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Watoto Tanzania Aidath Ishulula ameishukuru Serikali kwa utekelezaji wa Haki ya kuishi kwa mtoto kuanzia tumboni kwa kuhakikisha kunakuwa na zahanati na vituo vya afya vinavyosaidia kuwapatia huduma za afya watoto na wakinamama.
“Niseme Serikali imefanikisha kutupatia watoto haki ya kuishi kwa kushirikiana na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kwa kuhakikisha huduma za afya kwa Mama na mtoto zinapatikana kwa urahisi na kwa karibu hii itasaidia kuwa na Tanzania imfaayo kila mtoto kuishi” alisema
Akitoa mafunzo hayo Maalum kwa watoto Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bi. Mwelinde Kato amesisitiza kuwa Serikali imeanzisha Sera ya Mtoto ya mwaka 2008, Sheria ya Mtoto ya Mwaka 2009 na Mpango mkakati wa taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto ambavyo vinasukuma jamii kuhakikisha inazingatia na kutekeleza masuala mbalimbali yahusuyo watoto ikiwemo kupata haki zao za msingi zitakaziwezesha ustawi wao.
Ameongeza kuwa jamii ina nafasi kubwa katika kuhakikisha mtoto anapata haki zake za msingi zikiwemo Haki ya kuishi, kulindwa, kuendelezwa, kushirikishwa na kutobaguliwa ambazo zitaleta chachu kwako katika kuwa na taifa lenye watoto imara watakaoliendeleza taifa.
Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bw. Juma Samuel amesisitiza jamii hasa wazazi na walezi kuwawasidia watoto kuondokana na vitendo vya ukatili kwani chanzo kikubwa cha vitendo hivyo huanzia nyumbani.
“Jamii iwe chanzo cha kuondokana na vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa ni vitendo hivi vinatokea hasa katika jamii zetu tupambane dhidi ya vitendo vya kikatili kwa watoto wetu” alisema