Home Mchanganyiko RC.MAKONDA AKABIDHI VIFAA TIBA HOSPITAL YA KIVULE NA KIGAMBONI

RC.MAKONDA AKABIDHI VIFAA TIBA HOSPITAL YA KIVULE NA KIGAMBONI

0

******************************

Na Magreth Mbinga

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam amekabidhi vifaa tiba katika hospitali ya Kivule iliyopo Manispaa ya Ilala na Hospitali ya Kigamboni .

Makabidhiano hayo yamefanyika Leo Ofisini kwake Ilala Jijini Dar es Salaam katika Wilaya hizo mbili.

RC Makonda amesema vifaa hivyo ni vitanda Mia sita , magodoro miasita na mashine za kusaidia kupumulia Saba.

Pia Mkuu wa Wilaya ya Ilala Dk Sophia Mjema amemshukuru Rc Makonda na Mh Rais John Magufuli kwa kutekeleza ahadi ambayo waliitoa kwa kujenga hospitali hiyo.

“Naomba nitoe shukrani kwa Mh Rais na RC kwa kutekeleza ahadi na Leo wamenikabidhi vitanda miatatu,magodoro miatatu na mashine mbili za kupumulia”amesema DC Mjema.

Vilevile DC wa Kigamboni Mh Sara Msafiri ameshukuru Serikali ya awamu ya tano kwa kutekeleza ahadi yake katika Wilaya hiyo kwa ujenzi wa hospitali hiyo.

“Kwaniaba ya wanakigamboni napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa kupata vitanda miatatu,magodoro miatatu na mashine tano za kusaidia kupumulia kwa wagonjwa.

Sanjari na hayo Maganga Mkuu wa Mkoa Dk Rashidi Mfaume ameshukuru Serikali kwa kuwaangaliao sekta ya afya kw kuendelea kuwaunga mkono toka kipindi cha Corona hadi sasa.

Vilevile Maganga Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Dk Charles Mkombachepa amemshukuru ishikuru Serikali kwa kuwakumbuka Wilaya ya Kigamboni kwa kuwajengea hospitali na umeanza kufanya kazi tar 1 mwezi huu wa 6.