Home Mchanganyiko ABIRIA 13 WANUSURIKA KIFO BAADA YA BASI KUTUMBUKIA MTO ICHUNILO NJOMBE

ABIRIA 13 WANUSURIKA KIFO BAADA YA BASI KUTUMBUKIA MTO ICHUNILO NJOMBE

0

*****************************

NJOMBE

Abiria 13 waliokuwa kwenye basi la kampuni ya Dosmeza lenye namba za usajiri T 802,DEZ linalofanya safari zake katika mikoa ya Iringa wamenusurika kifo baada ya kuacha njia na kutumbukia katika daraja la mto Ichunilo mkoani Njombe .

Mara baada ya kutokea ajali hiyo majeruhi waliokolewa na walikimbizwa katika hospitali ya mji wa Njombe Kibena ambapo mganga mfawidhi wa hospitali hiyo Dr Alto Mtega anasema amepokea majeruhi 13 na kuwapa huduma ya kwanza lakini wawili wamepata majeraha makubwa ikiwa ni pamoja na kuvunjika mishipa ya shingo.

Dr Mtega amesema mapema baada ya kupokea majeruhi walianza kutoa huduma ya kwanza lakini mejuruhi wawili watapatiwa huduma za awali na kisha watatoa rufaa ili wakapatiwe matibabu zaidi Muhimbili.

Kituo hiki kimelazimika kufunga safari hadi hospitali ya Kibena na kuzungumza na baadhi ya majeruhi akiwemo Hussein Msakuzi,Frorida Mdemu ambao wanasema wanaendelea vizuri na kumshushia pongezi dereva kwamba amepambana sana kunusuru maisha yao kuanzia mwanzo wa mlima hadi kona ya mwisho ya mtereko wa Ichunilo.

Nae kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Njombe Hamis Issah anathibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kudai kwamba uchunguzi wa awali unaonyesha basi liliacha njia kutokana na mwendo mkali na kutoa rai kwa madereva kuwa makini katika eneo hilo lenye kona nyingi na mteremko mkali.

Baadhi ya waokoaji wakitafuta watu ndani ya mto akiwemo Ezekiel John wanasema jitihada kubwa zimefanyika kwa kushirikiana na jeshi la polisi na zimamoto ambao wanadaiwa kufika eneo la tukio dakika tano baada ya tukio na kuwaokoa majeruhi wote na kisha kuwakimbiza hospitali ya mji wa Njombe .