Katibu Mkuu, Wizara ya Maji Prof. Kitila Mkumbo akizindua eneo la kunawa mikono katika kukabiliana na maambukizi ya Virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Corona (COVID-19) katika shule ya sekondari ya Tumaini, mkoani Singida ambapo wanafunzi zaidi ya 100 wanajiandaa kwa mtihani wa kidato cha Sita. Kulia kwake anayeshuhudia ni Mkuu wa wilaya ya Iramba Emmanuel Luhahula.
Katibu Mkuu, Wizara ya Maji Prof. Kitila Mkumbo akiongea na wanafunzi wa shule ya sekondari ya Tumaini wanaojiandaa na mtihani wa kidato cha Sita ambao amewakabidhi vitakasamikono ambavyo kila mmoja ataweza kutumia kwa muda wa siku 60. Aidha, jumuiya ya shule hiyo pia ameikabidhi miundombinu ya kunawa mikono
Katibu Mkuu, Wizara ya Maji Prof. Kitila Mkumbo (kushoto) akimkabidhi mmoja wa wafanyakazi wa shule ya sekondari ya Tumaini vitakasamikono kwa niaba ya jumuiya ya shule hiyo katika hafla fupi ya kukabidhi miundombinu ya kunawa mikono na vitakasamikono iliyofanyika shuleni hapo.
Sehemu ya vitakasamikono ambavyo wanafunzi wa shule ya sekondari ya Tumaini, mkoani Singida wamekabidhiwa . Vitakasamikono hivyo vimeandaliwa Idara ya Ubora wa Maji, Wizara ya Maji, ni moja ya mchango wa sekta ya maji katika mapambano dhidi ya kujikinga na maambukizi ya Virusi vinavyosababisha ugonjwa wa COVID-19.