Home Mchanganyiko WANANCHI ZANZIBAR WAIOMBA ZEC KUANDAA UTARATIBU KUWAPA NAFASI WALIOKOSA KUJIANDIKISHA BAADA YA...

WANANCHI ZANZIBAR WAIOMBA ZEC KUANDAA UTARATIBU KUWAPA NAFASI WALIOKOSA KUJIANDIKISHA BAADA YA KUKOSA VITAMBULISHO KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

0

wananchi wa wilaya ya wete wakiwa katika ofisi ya vizazi na vifo walikusbiri kuchuua vitambulisho vya Mzanzibar mkaazi

picha na masanja mabula

*********************************

Na Masanja Mabula,PEMBA.

WANANCHI waliokosa nafasi ya kuandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura kutokana na kutopata vitambulisho vya Mzanzabari mkaazi wameiomba Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar-ZEC-kuandaa utaratibu ili wapate fursa hiyo ya kidemokrasia.

Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi wamesema kukosa fursa ya kujiandikisha inawanyima haki ya kuchagua kiongozi wanayemtaka.

Wamesema kwamba pamoja na changamoto iliyojitokeza juu ya upatikanaji wa vitambulisho hivyo ,lakini baada ya kuvipata wanahitaji kuwemo kwenye daftari hilo ili hapo baadaye washiriki uchaguzi Mkuu.

Omar Shaame alisema ni vyema utaratibu ukaandaliwa ili kuhakikisha wanaandakisha lengo ni kushiriki uchaguzi hapo baadaye”alisema.

Mbasho Juma mkaazi wa Mtambwe aliwataka wananchi kuacha kuilamu tume ya uchaguzi juu ya vitambulisho , wanachaotakiwa ni kushauri zoezi la uwandikishaji lifanyike japo kwa siku moja.

Alisema vitambulisho vinaendelea kutolewa na kila mwenye sifa anapata lakini changamoto ni muda wa zoezi umemalizika.

“Tunatakiwa kuishauri Tume kurejea zoezi japo siku moja ili na waliokosa kwa awamu hii waweze kupata fursa ya kuandikishwa”alishauri.