Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe akizungumza wakati wa utiaji wa saini ya mkataba kati ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (USCAF) katika Hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Mkurugezi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) Bw. Waziri Kindamba na Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote, Bi.Justina Mashiba wakisaini nyaraka za mkabata wa thamani zaidi ya bilioni tano kwa TTCL kupeleka mawasiliano vijijini katika Hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam na kuhuhudia na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe pamoja na Katibu Mkuu wa Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano Sekta ya Mawasiliano Dkt. Zainab Chaula
Mkurugezi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) Bw. Waziri Kindamba na Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote, Bi.Justina Mashiba wakibadilishana hati mara baada ya kusaini mkataba katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
*********************************
NA EMMANUEL MBATILO
Takribani wakazi laki 521,897 waishio vijijini wanatarajiwa kupelekewa huduma ya mwasiliano kupitia mpango wa upelekaji wa huduma ya mawasiliano katika maeneo yenye mawasiliano hafifu.
Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe wakati wa hafla ya utiaji saini mkataba wa mradi huo kati ya Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) na Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) iliyofanyika katika ofisi za Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Jijini Dar es Salaam.
Amesema mradi huo utanufaisha kata 32 zenye vijiji 45 katika maeneo ya mipakani na Kanda Maalumu kwa gharama za shilingi Bilioni 5.1, ikiwa ni utekelezaji wa awamu ya tano ya mradi huo.
“Ninashauku kubwa kuona huduma zote wanazofurahia watu wa mijini ikiwemo kupiga na kupokea simu,kutuma na kupokea fedha na matumizi ya mtandao wa intaneti zinawafikia pia watu wa vijijini kabla ya kumalizika mwaka 2021”. Amesema Mhandisi Kamwelwe.
Amesema kuwa Serikali kupitia UCSAF imefanikiwa kufikisha huduma za mawasiliano kwa wananchi wengi awali hawakuwa na huduma hiyo muhimu.
Aidha Mhandisi Kamwelwe ameitaka NEMC kuharakisha mchakato wa kupatikana kibari cha mazingira ili mradi huo uweze kutekelezwa kwa haraka.
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote, Bi.Justina Mashiba alisema mfuko hadi sasa umeshatekeleza miradi 302.
“Jumla ya sh. Bilioni 60 zilitokewa kama ruzuku kwa TTCL kupeleka mawasiliano vijijin na kuongeza kuwa hadi sasa mfuko umetenga ruzuku ya sh. Milioni 150.9 kwa ajili ya mradi huo”. Amesema Bi.Justina
Hata hivyo amesema mawasililiano ndio chachu ya maendeleo hivyo husaidia ukuaji wa uzalishaji wa viwanda.
kwa upande wake Mkurugezi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) Waziri Kindamba amesema Mradi huo utakapokamilika utaleta tija katika kuchangia maendeleo ya wananchi na taifa letu kwa ujumla.
Shirika la Mawasiliano TTCL limeendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya ujenzi wa mawasiliano katika maeneno ambayo hayana mvuto wa kibiashara
“Ukipita kwenye saiti mbalimbali mafundi wetu wapo kazini tunahakikisha miradi hii tunaitekeleza ili wananchi waweze kuwasiliana na huu mradi tutahakikisha tunajitahidi kuweza kuukamilisha kwa wakati ili wananchi ili waweze kuwasiliana”. Amesema Bw.Kindamba