Mkuu
wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella katika akikata utepe leo kuashiria
uzinduzi wa kituo cha kuweka mafuta kinachoendeshwa na kampuni tanzu ya
shirika la maendeleo ya Petroli Tanzania ( Tan Oil.) kushoto ni
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania
(TPDC),Dk James Mataragio na kulia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga
Henry Shekifu uzinduzi huo ulifanyika kijiji cha Michungwani kata ya
Segera wilayani Handeni
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella katika akikata utepe leo
kuashiria uzinduzi wa kituo cha kuweka mafuta kinachoendeshwa na kampuni
tanzu ya shirika la maendeleo ya Petroli Tanzania ( Tan Oil.) kushoto
ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania
(TPDC),Dk James Mataragio na kulia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga
Henry Shekifu uzinduzi huo ulifanyika kijiji cha Michungwani kata ya
Segera wilayani Handeni
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania
(TPDC),Dk James Mataragio akizungumza wakati wa uzinduzi huo kushoto ni
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kulia ni Mkuu wa wilaya ya
Handeni Godwin Gondwe
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akizungumza wakati wa uzinduzi huo kulia ni Mkurugenzi
Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC),Dk James
Mataragio kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Henry Shekifu
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Henry Shekifu akizungumza wakati wa uzinduzi huo
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi(CCM) wilaya ya Handeni,Athumani Malunda akizungumza wakati wa uzinduzi huo
MKUU wa wilaya ya Handeni Godwin Gondwe akizungumza wakati wa uzinduzi huo
AFISA wa Serikali za Mitaa Mkoa wa Tanga Gibson George akizungumza jambo kwenye uzinduzi huo
Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC),Dk James
Mataragio,Mkuu wa wilaya ya Handeni Godwin Gondwe na kulia ni Mwenyekiti
wa CCM Mkoa wa Tanga Henry Shekifu
wa Mkoa wa Tanga wametakiwa kuchangamkia fursa za kiuchumi na
kibiashara ambazo zinaletwa na Shirika la Maendeleo ya Petroli
Tanzania(TPDC) kupitia miradi yake katika sekta ya mafuta na gesi ambayo
inakuja mkoani humo.
Hayo yamebaishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa
Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC),Dk James Mataragio
pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigela jana katika kijiji cha
Michungwani kata ya Segera wilayani hapa katika hafla fupi ya uzinduzi
wa kituo cha kuweka mafuta kinachoendeshwa na kampuni tanzu ya shirika
hilo Tan Oil.
Akizungumza katika hafla hiyo,Dk Mataragio amesema
kuwa shirika hilo limeingia rasmi katika mkakati wake wa kufufua
biashara ya mafuta ambayo ilikuwepo tangu shirika hilo lilipoanzishwa
mwaka 1969 kabla ya kusitisha huduma hizo.
Amesema
kuwa mkakati huo sio lengo la serikali kuua kampuni binafsi za mafuta
bali ni kuingia katika ushindani wa biashara ya mafuta ikiwemo uagizaji
wa mafuta kupitia mfumo wa pamoja wa uagizaji wa mafuta(BPPA),kudhibiti
bei ya mafuta ,kuwa na takwimu za matumizi ya nishati hiyo pamoja na
usambazaji kwa ujumla.
Amesema kuwa wanatarajia kuzindua vituo
vingine sita vya aina hiyo baada ya kuzindua vituo vingine viwili Musoma
mkoani Mara na Segera wilayani Handeni mkoani hapa.
Aidha,amesema
kuwa katika kipindi cha miaka mitano ijayo Shirika hilo litajenga vituo
vingine 100 katika maeneo mbalimbali nchini katika Halmashauri za
Wilaya sambamba na ujenzi wa matenki makubwa ya kuhifadhia mafuta katika
mikoa mbalimbali hapa nchini.
huyo aliitaja mikoa hiyo kuwa ni Tanga,Dar es
salaam,Morogogo,Dodoma,Mbeya na Isaka-Kahama kwa kushirikiana na Mamlaka
ya Bandari nchini(TPA) ili kuunguza msongamano wa wfanyabiashara
kuchukua mafuta sehemu moja pamoja na kupunguza misongamano ya magari
lengo likiwa ni kulinda miundombinu ya barabara.
“TanOil
inachukua kazi zote za iliyokuwa kampuni ya mafuta ya Copec sasa
tunaingia rasmi katika biashara ya mafuta, lengo si kuziondoa kampuni
binafsi za mafuta bali ni kuleta ushindani, kudhibiti bei, kuwa na
takwimu sahihi za mafuta na kuagiza mafuta kwa ujumla (BPPA),” alisema.
Kuhusu
ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima-Uganda hadi Chongoleani
jijini Tanga,amesema kuwa baada ya kampuni ya Tullow kuwauzia hisa zao
kampuni ya mafuta ya Total,sasa kampuni hiyo itamiliki hisa hizo kwa
asilimia 66.7 na wamefikia muafaka na mradi utaanza mapema mwakani .
Amefafanua
kuwa katika kipindi cha mwezi Juni,wataanza kutangaza zabuni za ujenzi
wa mradi kwa kampuni mbalimbali,mwezi Desemba watapitia kampuni hizo ili
kujua gharama za mradi na ujenzi wa mradi huo utasimamiwa na Shirika la
Mafuta la Uganda(NOC),Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania(TPDC) na
kampuni ya CNOOC.
“Ujenzi wa bomba la mafuta uliokuwa uanze
ulikwamishwa na mazungumzo ya kodi kati ya kampuni za mafuta kwa hiyo
kuanzia mwaka huu mwezi Jui tutaanza kutangaza zabuni hadi mapema
mwakani kazi zitaanza,hivyo wananchi wa mkoani Tanga kupitia miradi ya
TPDC changamkieni fursa za kiuchumi na biashara,”alisema.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi huo ,Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigela
aliwashukuru TPDC kwa kuanzisha vituo hivyo mkoani humo nawataka
wananchi kutoa ushirikiano wa ulinzi katika vituo hivyo kutokana ni mali
ya serikali na kuwasisitiza kuanzisha shughuli za uwekezaji zaidi na
kjipatia fursa za ajira kupitia miradi ya TPDC ikiwemo kufunguliwa vituo
vya mafuta,gesi na mradi mkubwa wa bomba la mafuta ghafi(EACOP).
Pia,
amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga, Daudi Mayeji
kuharakisha mchakato wa taarifa ya tathmini ya eneo ambalo TPDC
watajenga tenki kubwa la kuhifadhia mafuta ili wananchi walipwe fidia na
ujenzi uanze haraka.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe
amesema kuwa katika mradi wa bomba la mafuta(EACOP)wilaya hiyo inapitiwa
na bomba hilo kwa urefu wa kilometa 54,na eneo la kambi kubwa
itakayojengwa Handeni lina ukubwa wa ekari 51 na tayari wananchi wa
Misima wamekubali kuondoka kupisha ujenzi huo.
Kuhusu ujenzi wa
vituo vya mafuta vya TPDC,amesema wilaya hiyo ina maeneo mengi ya
uwekezaji hivyo amekubali kutoa eneo popote pindi TPDC wakitaka kwa
ajili ya ujenzi huo.
Awali Mwenyekiti wa Chama cha
Mapinduzi(CCM) wilaya ya Handeni,Athumani Malunda aliwaomba TPDC kujenga
vituo vingine viwili kama hivyo wilayani humo katika maeneo ya Mkata na
Handeni mjini na kumtaka Mkurugenzi Mtendaji ikibidi kuwapa eneo.