Home Mchanganyiko TBL Plc yatoa vifurushi vyenye vifaa vya kujikinga na Covid 19...

TBL Plc yatoa vifurushi vyenye vifaa vya kujikinga na Covid 19 kwenye mabaa nchini.

0

Katika mkakati wake wa kuunga mkono jitihada za Serikali za kukabiliana na maambikizi ya ugonjwa wa Covid 19, kampuni ya bia ya TBL, imetoa vifurushi vyenye vifaa vya kujikinga na ugonjwa huo kwenye mabaa zaidi ya 2,500 nchini pote kwa ajili ya wahudumu na wateja.Vifaa hivyo vimezalishwa nchini na ubora wake kuthibitishwa.

Afisa Mauzo wa TBL,Catherine Lyakurwa akikabidhi vifaa kwenye baa ya Africana mini Arusha

Meneja Mauzo wa TBL Plc, Silvanus Musomi (kulia) akimkabidhi Meneja wa baa ya Calabash     iliyopo Mwenge   jijini Dar es Salaam, Kiringa Wanzagi

Meneja Mauzo wa Kanda ya nyanda ya Kusini kutoka Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Abubakar Masoli (kulia) akikabidhi vifaa kwenye baa ya Mwailubi mjini Mbeya.

Mbeya Carnival nayo imefikiwa na mgao wa vifurushi hivyo vya kinga

Meneja Mauzo wa TBL mkoa wa Mwanza, Issa Makani akiwapatia vifaa via kinga wahudumu wa Bar ya Chanya ya jijini Mwanza