Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini, Mhe. Anthony Mavunde,akiwa kwenye gari kabla ya kuzungumza na wananchi wa eneo la Mbuyuni Kata ya Kizota Mkoani Dodoma wakati wa zoezi la uwekaji bikoni katika makazi hayo.
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini, Mhe. Anthony Mavunde,akicheza ngoja kabla ya kuweka zoezi la uwekaji bikoni katika makazi ya wananchi wa eneo la Mbuyuni Kata ya Kizota .
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini, Mhe. Anthony Mavunde,akizungumza na wananchi wa eneo la Mbuyuni Kata ya Kizota Mkoani Dodoma wakati wa zoezi la uwekaji bikoni katika makazi hayo.
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini, Mhe. Anthony Mavunde,akisisitiza jambo kwa wananchi wa eneo la Mbuyuni Kata ya Kizota Mkoani Dodoma wakati wa zoezi la uwekaji bikoni katika makazi hayo.
Sehemu ya wananchi wakimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini, Mhe. Anthony Mavunde,wakati akizungumza kabla ya zoezi la uwekaji bikoni katika makazi hayo.
Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Godwin Kunambi,akizungumza na wananchi wa eneo la Mbuyuni Kata ya Kizota Mkoani Dodoma wakati zoezi la uwekaji bikoni katika makazi hayo.
Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Godwin Kunambi,akisisitiza jambo kwa wananchi wa eneo la Mbuyuni Kata ya Kizota Mkoani Dodoma wakati zoezi la uwekaji bikoni katika makazi hayo.
Mkurugenzi wa Global Suvery .Co.Ltd Bw.Msungu Daudi,akizungumza na wananchi wa eneo la Mbuyuni Kata ya Kizota Mkoani Dodoma wakati zoezi la uwekaji bikoni katika makazi hayo.
Diwani wa Kata ya kizota Comrede Jamal Ngalya,akizungumza na wananchi waeneo la Mbuyuni Kata ya Kizota Mkoani Dodoma wakati zoezi la uwekaji bikoni katika makazi hayo.
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini, Mhe. Anthony Mavunde,akiwa na Mkurugenzi wa jiji la Dodoma Godwin Kunambi wakikata utepe wa uzinduzi wa zoezi la uwekaji bikoni katika eneo la Mbuyuni Kata ya Kizota Mkoani Dodoma.
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini, Mhe. Anthony Mavunde,akiwa na Mkurugenzi wa jiji la Dodoma Godwin Kunambi akizindua rasmi zoezi la uwekaji bikoni katika eneo la Mbuyuni Kata ya Kizota Mkoani Dodoma.
………………………………………………………………………….
Na.Alex Sonna,Dodoma
Wananchi wa Kata ya Mbuyuni Mkoani Dodoma warasimishiwa rasmi makazi yao baada ya mgogoro uliyodumu kwa muda mrefu.
Hayo yamebainishwa leo na Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini, Mhe. Anthony Mavunde wakati wa zoezi la uwekaji bikoni katika makazi hayo.
Aidha Mhe. Mavunde amesema kuwa katika makazi hayo kuna eneo limetengwa kwa ajili ya kujenga Shule ya Msingi ili kuwa hudumia watoto katika makazi hiyo.
“Kwa kazi kubwa aliyoifanya Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Bw. Godwin Kunambi natoa wito kwa baraza la madiwani shule ya msingi itakayojengwa katika kata hii iitwe Shule ya Msingi Kunambi ili kutambua utendaji kazi wake katika kufanyikisha urasimishaji wa makazi haya”, ametoa rai Mhe. Mavunde.
Pia Mhe. Mavunde amesema kuwa yeye kama kiongozi wa Wanachi wa kata ya Mbuyuni waliyompa dhamana ya kuwa kiongozi wao ameahidi kujenga darasa moja katika shule hiyo kama sehemu ya kutoa shukrani kwa wanachi wake.
Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Ndg. Godwin Kunambi amewataka wananchi wao kuhakikisha wanalipia malipo ya kisheria mapema ili zoezi la kumilikishwa likamilike kiurahisi na kuahidi kuboresha miundombinu ya barabara pamoja na huduma nyingine muhimu sambamba na ujenzi mpya wa Shule ya Msingi.
Naye Mkurugenzi wa Global Suvery .Co.Ltd Bw.Msungu Daudi ambaye kampuni yake imepewa jukumu la nupimaji wa eneo hilo amesema kuwa kazi hiyo itakamilika ndani ya miezi mitatu .
“Katika kutekeleza kazi hii katika kata ya Mbuyuni Vijana wa hapa watapata ajira ili nawao kuweza kupata kipato cha kujikimu wao na familia zao,” ameeleza Bw. Daudi
Kwa upande wake mwananchi wa Kata ya Mbuyuni, Bi. Hafsa Kassa akitoa neno la shukrani kwa niaba ya wananchi kata hiyo amesema kuwa anawashukuru viongozi wote kwa ushirikiano waliyokuwa nao katika kufanyikisha kuwapatia makazi wote wakiwa chini ya mwamvuli wa Mhe. Rais, wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.