Home Mchanganyiko RIDHIWANI KWA KUSHIRIKIANA NA STABIC BANK WASHUSHA NEEMA KITUO CHA AFYA MIONO

RIDHIWANI KWA KUSHIRIKIANA NA STABIC BANK WASHUSHA NEEMA KITUO CHA AFYA MIONO

0

******************************

NA MWAMVUA MWINYI,CHALINZE
MBUNGE wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwan Kikwete, amekabidhi vifaa tiba katika kituo cha afya cha Miono,Mkoani Pwani vilivyotolewa kwa hisani ya taasisi ya kifedha ya Stanbic.
Akikabidhi vifaa hivyo kwa mkurugenzi wa halmashauri ya chalinze,alisema vifaa hivi vitakuwa neema na mkombozi kwa mahitaji wa afya kutokana na baada ya ukamilikaji wa chumba cha Upasuaji ambacho kitahudumia wananchi wa maeneo hayo hususan wakina mama wakati wa kujifungua na huduma za upasuaji.
“Nimekuwa nikikosa usingizi nilipoona kituo hiki cha Miono kinasuasa kwisha. Lakini nashukuru Serikali kupitia Halmashauri yetu imetoa pesa na sasa kituo kipo hatua ya mwisho ya ujenzi.” 
Ridhiwani hakusita kumshukuru Rais John Magufuli na serikali ya awamu ya Tano kwa namna inavyoendelea kuimarisha afya za wananchi kwa kuwapatia zaidi ya sh. Bilioni 1.7 ambazo Zimetumika kwa ajili ya miradi mbalimbali ya Kuimarisha afya katika kata mbalimbali za halmashauri hiyo .
“Ujenzi wa kituo cha afya cha kiasasa Kata ya kibindu, kituo cha Afya cha Lugoba, Miradi ya upanuzi wa kituo cha Afya Chalinze sanjari na ujenzi wa Maabara kubwa ya damu, kituo cha ushauri nasaha Mdaula na Zahanati ya Kijiji cha Mdaula” alibainisha Ridhiwani.
Nae Meneja wa Stanibic Bank ,Richard Chenga alimpongeza mbunge huyo kwa jinsi anavyokuwa mstari wa mbele kuwasemea watu wake na jinsi anavyovumbua miradi yenye tija kwa wananchi wake. 
Alizitaka taasisi nyengine nchini kuunga mkono juhudi za serikali  katika kusaidia jamii ususani ni uyaratibu wa kutoa magawio kwa wananchi ili kuunga mkono serikali  katika utekelezaji wake wa miradi.
Halima Juma,ni mkazi wa Miono alimpongeza Mbunge Ridhiwani kwani kwa kufanya hivyo wakina mama wa watakuwa wanajifungua bila matatizo.