………………………………………………………………………………..
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brigedia Generali Mstaafu Nikodemas Mwangela amefanya ziara ya siku moja katika Halmashauri za Tunduma na Mbozi kwa kuwatembelea wakulima wa Mahindi na kahawa katika Mashamba yao.
Mkuu huyo wa Mkoa aliianza ziara yake kwa kuwatembelea wakulima wa Mahindi kata Chiwezi iliopo Mji wa Tunduma ambapo aliweza kukutana na Baadhi ya wakulima wakubwa wa zao hilo la Mahindi.
Wakulima waliweza kumueleza Changamoto mbalimbali wanazokutana nazo ” Mh Mkuu wa Mkoa tunakuomba sana utusaidie uwezekano wa kupata matrekta ya mkopo uwezo wa kulipa sisi tunao lakini hatujui tuanzie wapi kukopa” aliyasema hayo Mkulima wa Mahindi Elia Mwakabenga
Ziara ilihamia katika Wilaya ya Mbozi ambapo Mkuu wa Mkoa aliweza kuwatembea wakulima wa Zao la kahawa katika Shamba kubwa la Kanji Lanji walimuonyesha jinsi wanavyoiandaa kahawa nayo toka wanavyochuma mpaka wanavyoikoboa pia.
“Mh Mkuu wa Mkoa Changamoto kubwa tulio nayo hapa ni umeme tuna mitambo mikubwa ambayo inahitaji Umeme mfano CPU yetu inatulazimu tutumie Lita 25000 za disel kila mwaka”-Jacob Swai Meneja Kanji Lanji.
Aidha Mkuu huyo wa Mkoa aliwata wakulima kuuza Mazao yao kwa bei ya juu na kutokubali kuuza kwa bei ya chini na amewapongeza kwa kufanya kilimo bora