**********************************
NA EMMANUEL MBATILO
Chama cha TLP chini ya Mwenyekiti wake Augustine Lyatonga Mrema kimempokea mwanachama mpya aliyekuwa Mwenyekiti wa Jimbo la Manyoni Mashariki (CHADEMA) ambaye pia alikuwa mgombea Ubunge wa jimbo hilo Bw.Emmanuel David Allute kutokana na chama hicho pekee cha upinzani kumuunga mkono Rais Dkt.John Pombe Magufuli.
Akizungumza na Wanahabari katika Makao Makuu ya Ofisi ya Chama hicho jijini Dar es Salaam,Mwenyekiti wa Chama cha TLP-Taifa, Bw. Augustine Mrema amefungua milango wazi kwa wanachama kujiunga na chama hicho ambao watakuwa tayari kumuunga mkono Rais Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli.
“Niwaombe wale wanachama wa TLP waliodanganywa na kukihama chama hiki wakiamini chama kimekufa, Chama hiki hakifi angalia tulivyowekeza sasa, tunawekeza kwa watu mashuhuri na wasomi na wenye nguvu”. Amesema Bw.Mrema.
Kwa upande wake Mwanachama mpya wa chama hicho Bw.Allute amesema kuwa Chadema imeshapoteza dira na mwelekeo kwani kuna baadhi ya viongozi wa chama hicho wamekifanya chama kuwa mali binafsi wakati fulani Mhe.Freeman Mbowe (Mb) alisikika akisema “Hiki chama ni mali yangu binafsi”.
Pamoja na hayo Bw.Allute amesema kuwa juhudi zilizofanywa na Rais Dkt.John Pombe Magufuli ni kubwa na pia zimevunja rekodi hivyo anastahiri pongezi.
“Tangu Uhuru hatujawahi kupata Rais aliyenunua ndege 6 keshi, hatujawahi kupata Rais anayejenga SG yenye kutoa 2,100MW,Rais anayejenga zaidi ya KM 2,000 za SGR, Rais anaejenga zaidi ya KM 4,000 za lami hivi sasa.Mambo haya ndo yamenileta TLP-Tanzania ili kushirikiana na wenzangu tuhakikishe Rais Magufuli anashinda kwa kishindo Octoba 2020 ili aendelee kutupa eaha zaidi”. Amesema Bw.Allute.