Home Mchanganyiko TCCO NA MIRACLE FEET WATOA SHUKRANI KWA HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA...

TCCO NA MIRACLE FEET WATOA SHUKRANI KWA HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA MBEYA KWA MATIBABU YA WATOTO WENYE MATATIZO YA MIGUU NYANDA ZA JUU KUSIN 

0

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali Ya Rufaa ya Kanda Mbeya Dkt Godlove Mbwanji akipokea cheti cha shukrani kutoka kwa Mratibu Msaidizi wa TCCO Nyanda za Juu Kusini Bi. Ainael Sarinjo, kushoto ni kiongozi wa Idara ya Phiziotherapi PT. Seraphine Mushi.

…………………………………………………………………………………….

Taasisi inayo toa huduma kwa watoto wenye ulemavu wa mguu kifundo (TCCO) kwa kushirikiana na Shirika la msaada kwa watoto wenye nyayo zilizopinda (clubfoot) – MIRACLE FEET leo wamekabidhi cheti cha shukrani kwa hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya kwa kuendelea na utoaji wa huduma za matibabu ya watoto wenye tatizo la miguu kifundo kwa Nyanda za Juu Kusini.

Akikabidhi cheti hicho Mratibu Msaidizi wa TCCO Nyanda za Juu kusini, Bi. Ainael Sarinjo ameipongeza hospitali kwa hatua ilizozichukua katika kukabiliana na janga la virusi vya CORONA huku wakiendelea kutoa huduma kwa watoto wenye miguu kifundo.

Amesema kuwa Taasisi yao wameridhishwa na kufurahishwa na hospitali kutositisha huduma za matibabu kwa watoto wenye miguu kifundo kwasababu tu ya CORONA.

Aikipokea Cheti hicho kwa niaba ya viongozi na watumishi wa hospitali ya MZRH, Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali Dkt. Godlove Mbwanji ameishuukuru Taasisi ya TCCO kwa kutambua mchango mkubwa unaofanywa na watumishi wa hospitali hasa katika idara ya Phisiotherapi kwa kuona kwamba matibabu kwa watoto ni lazima yaendelee hata katika kipindi hiki cha COVID 19.

“Tunaishukuru sana TCCO kwa kutambua mchango wa hospitali yetu kuliona hili, nasi tunarudisha pongezi hizi kwa Mh. Raisi John Pombe Makufuli kwa sababu katika ngazi ya Taifa katutia moyo sana, na kufanya mambo yaendelee hata katikati ya hili janga ambalo limekua likiisumbua dunia nzima, na hii imefanya huduma za wagonjwa wengine ikiwa ni pamoja na watoto wenye mguu kifundo kuendelea kupata huduma kama inavyotakiwa” – Dkt Mbwanji.

Hospitalii ya Rufaa ya Kanda Mbeya inatoa huduma ya kliniki na matibabu ya miguu kifundo au nyayo zilizopinda ambao ni ulemavu unaotokana na matatizo ya mifupa na misuri ambayo ni wakuzaliwa nao na unaweza mpata mototo yeyote duniani.