Home Michezo AKILI ELFUTANO SHABIKI WA YANGA AIPONGEZA GSM

AKILI ELFUTANO SHABIKI WA YANGA AIPONGEZA GSM

0

**************************

Na Magreth Mbinga

Shabiki wa Young African Akili Jumanne maarufu kama Akili Elfutano amewapongeza viongozi wa klabu hiyo na mdhamini wake GSM kwa kutaka kuwapeleka sehemu wanayao stahili.

Amezungumza hayo leo na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam na kusema huu Ni wakati muhafaka wa kwenda kwenye mabadiliko.

Pia Akili amewataka mashabiki wa Klabu hiyo wahakikishe wanakuwa wanachama ili kuleta maendeleo katika klabu.

Vilevile amesema hatakuwa tayari kunivumilia Mtu yeyote anaetaka kurudisha klabu nyuma kimaendeleo na kusema kuwa wana Young African watapambana nae.

Sanjari na hayo Akili amemtaka mdhamini wao GSM kuwa na msimamo huo huo kwani watatokea watu ambao watawapiga Vita lakini wasiwajali.

Hatahivyo amewaambia Wana Young African Ni wakati wa kila mmoja kufikilia na kubuni kitu ambacho atakifanyia klabu hiyo na kuwaunga mkono wachezaji wakati wakiwa uwanjani.

Akili amemalizia kwa kuwashukuru mashabiki wa Young African ambao walivumilia wakati walipopita katika wakati mgumu mpaka sasa wanaelekea sehemu nzuri pia Mh Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Magufuli kuruhusu mchezo wa soka uendelee.