Home Mchanganyiko ANUSURIKA KWENDA RUMANDE BAADA YA KUDAIWA KUIBA MALI YA SERIKALI

ANUSURIKA KWENDA RUMANDE BAADA YA KUDAIWA KUIBA MALI YA SERIKALI

0

**************************

Na Masanja Mabula , Pemba.

Anayedaiwa kuiba mali ya serikali anusurika kwenda rumande ni baada ya kutimiza masharti ya dhamana katika mahakama ya mwanzo wete.

Mtuhumiwa huyo anafahamika kwa jina la Aksam Seif Amour miaka 27 wa Ukunjwi wilaya ya wete , amefikisha katika mahakama hiyo akikabiliwa na kosa la kuiba vespa ambayo ni mali ya Serikali.

Mbele ya hakimu wa mahakama hiyo hamad ali suleiman , mwendesha mashtaka koplo khamis mzee ameiambia mahakama kwamba , baina ya terehe 12/5/2020 majira ya saa kumi na nusu jioni na tarehe 13/5/2020 saa mbili na robo asuhubi, bila ya halali kijana huyo aliiba vespa ya yenye namba za usajili SMZ, 742 C , yenye thamani ya shilingi 2,200,000 kwa makisio mali ya serikali ya mapinduzi ya zanzibar.

Mtuhumiwa huyo  hakutakiwa kujibu lolote kwa vile mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi za aina hiyo na kesi imepangwa kusikilizwa juni 16 mwaka huu katika mahakama ya wilaya.

Na mtuhumiwa yuko nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti aliyopewa na mahakama ambapo ametakiwa kujidhamini mwenyewe kwa kiasi cha shilingi 1,500,000/ za maandishi na wadhamini wengine wenye kina kama hicho cha Pesa.