Home Mchanganyiko WAJASIRIAMALI ZANZIBAR WATAKIWA KUTOKATA TAMAA KATIKA HARAKATI ZA UZALISHAJI BIDHAA

WAJASIRIAMALI ZANZIBAR WATAKIWA KUTOKATA TAMAA KATIKA HARAKATI ZA UZALISHAJI BIDHAA

0

Mkurugenzi wa Chama cha waandishi wa habari wanawake Tamwa-Zanzibar Dkt,Mzuri Issa mara baada ya kuwasili katika moja ya shamba linalomikiwa na wajasiriamali wanawake huko Bumbwini Mkoa wa kaskazini Unguja ambapo shamba hilo limepangwa kutumika kwa kilimo cha mboga mboga.

 Baadhi ya wanakikundi kutoka shehia ya Bumbwini Mafufuni Unguja wakiendelea na shughuli zao za uzalishaji wa sabuni ya maji ambapo sabuni hizo zimekua na soko kubwa hisi sasa kufuatua kutumika kama kinga dhidi ya maradhi ya korona.

…………………………………………………………………..

Na Masanja Mabula , Zanzibar,

MKURUGENZI wa Chama cha waandisi wa habari wanawake Tamwa—Zanzibar Dr Mzuri Issa amewataka wajasiriamli kisiwani Unguja kutokata tamaa licha ya uwepo wa changamoto mbali   mbali katika harakati zao za kila za uzalishaji wa bidhaa.

Dkt,Mzuri aliyasema hayo jana wakati wa ziara maalumu ya kutembelea vikundi katika shehia mbali mbali za mkoa wa kaskazini kwa lengo la kujionea ni kwanamna gani wajasiriamali hao wanafanyia kazi elimu wanayopewa kupitia chama hicho.

Aliwataka wajasiriamali hao kutokata tamaa licha ya changamoto za hapa na pale badala yake wajitahidi zaidi wakiamini kuwa umoja wao ndio suluhisho la changamoto hizo.

Alisema kuna jitihada kubwa zimefanywa na wajasiriamali na wanapaswa kuungwa mkono kwa kuwa lengo lao ni moja kujikwamua na umasikini.

Aidha alisema Tamwa-Zanzibar itaendelea kufanya kila jitihada zenye lengo la kuhakiksha wanawasaidia wajasiriamali hao ili waweze kutimiza ndoto zao.

Katika hatua nyengine aliwataka wanawake kuzitumia fursa mbali mbali kwenye jamii ikiwemo za kushiriki mara pale muda utakapofika katika kugombe anafasi mbali mbali za kisiasa kupitia maeneo yao.

Aliwataka wanawake hao kuacha kubweteka na kudhani nafasi za uongozi ni za wanaume pekee badala yake wanapaswa kujitambua na kuwa tayari muda wowote.

Awali afisa uwezeshaji wanawake kiuchumi  Tamwa-Zanzibar Nairat Abdalla aliwataka akinamama hao kuridhika na masoko ya bidhaa zao katika maeneo husika badalka yake wanapaswa kufikiri mbali zaidi.

Alisema kuna fursa nyingi za masoko kupitia bidhaa hizo hivyo ni vyema kuyatumia mask ohayo ali waweze kujingizia kipato zaidi.

Kwa nyakati tofauti baadhi ya wajasiriamali hao walisema wamekua wakikumbana na ugumu katika utendaji wao wa kazi hususani za kilimo kutokana na maeneo mengi kukosa maji ambayo yangewafanya waweze kulima kwa urahisi katika kilimo cha mboga mboga.