Home Mchanganyiko LAKI MOJA YAMFIKISHA MAHAKAMANI MUUGUZI  ZAHANATI YA CHAMWINO 

LAKI MOJA YAMFIKISHA MAHAKAMANI MUUGUZI  ZAHANATI YA CHAMWINO 

0

 

Na. Alex Sonna, Dodoma

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoani Dodoma imemfikisha mahakamani muuguzi wa Zahanati ya Chamwino Zabron Richard ( 32) jijini Dodoma baada ya kuomba rushwa ya sh 100, 000 ili amsafishe kizazi mke wa mkazi wa eneo hilo.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoani Dodoma, Sosthenes Kibwengo wakati akizungumza na waandishi wa Habari.

Aidha Kibwengo amesema kuwa baada ya tukio hilo Takukuru iliweka mtego na kumbaini muuguzi huyo ambapo  ilimfikisha mahakamani kutokana na kosa hilo ambalo ni kinyume na sharia.

Kibwengo ameeleza kuwa muuguzi huyo alifanikiwa kuchukua sh 60, 000 baada ya kukamilisha kumsafisha mzazi huyo kizazi.

Kukamatwa kwa Muuguzi huyo kumekuja baada ya Mei 11 kupokea taarifa kutoka kwa mkazi wa Chamwino akihitaji huduma ya kusafishwa kizazi, lakini amekataliwa mpaka atoe sh 100, 000 wakati ni kinyume na sharia.

Mbali na hilo Takukuru Mkoani hapa inatarajia kumfikisha mahakamni Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Mpamatwa iliyopo wilayani Bahi Mkoani hapa  baada ya kukutwa na makosa manne ya rushwa.

Kibwengo alisema uchunguzi unaonyesha kwamba Juni 2019 Mtuhumiwa alighushi Mihutasari miwili ya vikao vya kamati ya shule na Mkutano wa walimu kuinyesha kwamba waliridhia kiasi cha sh 469, 500 kitolewe kwenye akaunti ya shule huku akifahamu kwamba ni uwongo na aliwasilisha mihutasari hiyo kwa Mkurugenzi wa halmashauri ya Bahi.

Katika hatua nyingine Takukuru imefanikiwa kuresha mashamba 13 ya wakazi wa kijiji cha Makole baada ya kutaifishwa kutokana na kuchukua mkopo wa riba kwa Nelson Ndalu.

Mashamba hayo yenye hekari 30 bwana Ndru maarufu kama Osama anakopesha kwa asilimia ya riba 100 ndipo akawapokonya mashamba hayo kutokana na kushindwa kulipa fedha walizolipa.

Baada ya Takukuru Kongwa kufanya uchunguzi wamebaini hiyo ni tabia ya Osama ya kudhulumu wakazi wa eneo hilo, ambapo Mei 7 ameridhia na kurejesha mashamba hayo.

Pia Takukuru Dodoma imefanikiwa kurejesha kiwanja namba tatu kitaluQ Iyumbu New Town Centre kwa Mkurugenzi wa jiji la Dodoma baada ya uchunguzi kubaini kwamba aliyekuwa Mhasibu wa CDA alimwezesha rafiki yake kupata kiwanja hiko kwa njia ya udanganyifu.

“Tumefanyia chunguzi na  kubaini jumla ya sh.milion 43, yalionekana malipo hayo yalifanyika 2016 na kukatiwa stakabadhi Januari 2017 wakati malipo ni batili na mtuhumiwa atafikishwa mahakamani”amesema Mkuu huyo.

Kibwengo pia ametoa onyo kwa Wajumbe wa Chama Cha Walimu (CWT) ngazi ya Taifa  kujiepusha na vitendo vya rushwa katika kuelekea Mkutano Mkuu wa Uchaguzi unatarajiwa kufanyika wiki hapa jijini Dodoma.

Kibwengo amesema kuwa wajumbe wa Mkutano huo wanapaswa kuzingatia taratibu za Chama Chao, Sheria za nchi na kujiepusha na vitendo vya rushwa na kuwa Katika mazingira ambayo yanaashiria uwepo wa vitendo hivyo.

“Natoa wito kwa wapambe wa wagombea wajihadhari na vitendo vya rushwa na kuepuka mazingira yenye viashiria vya rushwa kwani wanaweza kujikuta unakosa fursa ya kufanya kampeni au hata kutoshiriki uchaguzi,hatutaki tufike huko,”ametoa wito Kibwengo