Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni,Mhe. Benjamini Sitta akifuatilia hoja iliyokuwa ikiwasilishwa na Mkaguzi mkuu wa hesabu za nje, kulia ni Mkurugenzi Ndug. Aron Kagurumjuli
Baadhi ya madiwani na watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni wakiwa kwenye kikao cha Baraza la ukaguzi wa hoja za hesabu za Serikali.
Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za nje Manispaa ya Kinondoni Ndugu. liuther Msombola akisoma taarifa ya ripoti ya ukaguzi ya halmashauri hiyo wakati wa baraza la ukaguzi wa hoja.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni ,ndug. Aron Kagurumjuli akifungua kikao cha baraza la madiwani cha ukaguzi wa hoja za mkaguzi wa hesabu za serikali kilichofanyika leo katika ukumbi wa Manispaa. Kushoto ni Mstahiki Meya Mhe. Benjamini Sitta.
Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni wakiwa kwenye kikao cha baraza la madiwani la ukaguzi wa hoja za hesabu za serikali
*******************************
Manispaa ya Kinondoni imepongezwa kwa kupata hati safi kwa kipindi cha miaka mitano mfululizo katika hoja za ukaguzi wa hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha 2014/2015 hadi 2018/2019.rad
Pongezi hizo zimetolewa leo na Bi. Mary Assey kwa niaba ya Katibu Tawala Mkoa wa Dar es salaam wakati uchangiaji mada wa taarifa ya hoja za ukaguzi wa Hesabu za Serikali kwa mwaka 2018/ 2019 iliyowasilishwa na mkaguzi wa hesabu za nje Manispaa ya Kinondoni.
Bi. Mary amesema Kinondoni imeonesha uzalendo katika usimamiaji mzuri wa rasilimali za Serikali, hasa matumizi mazuri ya Fedha yanayoenda sambamba na thamani halisi ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kuzitaka Halmashauri nyingine kuiga mfano ya uendeshaji pamoja na usimamizi ili ziweze kuwa na mafanikio makubwa zaidi.
“ Ni wapongeze Kinondoni kwakupata hati safi kwa miaka mitano mfufulizo, hii inaonesha ni kwa kiasi gani Mkurugenzi Aron Kagurumjuli na timu yako mpomakini kwenye utendaji wenu, hasa usimamizi wa matumizi ya fedha kisera ,utekelezaji wa ilani sambamba na usimamizi mzuri wa miradi, tunazo Halmashauri tano katika mkoa wetu wa Dar es Salaam, lakini Kinondoni mnafanya vizuri, hongereni kwa hilo” amesema Bi. Mary.
Akitoa taarifa hiyo ya ukaguzi wa hesabu kwa mwaka 2018/ 2019, Mkaguzi Mkuu wa hesabu za nje Manispaa ya Kinondoni Ndg. Eliuther Msombola amesema kuwa ukaguzi huo umefanyika kwa mujibu wa ibara ya 143(2), ya katiba ya Jamuhuri ya Muungano w Tanzania ya mwaka 1977 (iliyorekebishwa mwaka 2005).
Aidha amefafanua kuwa lengo la ukaguzi huo ni kupata uthibitisho wa kuridhia kama taarifa za fedha kwa ujumla wake hazina makosa makubwa yanayotokana na udanganyifu au makosa ya kawaida.
Awali akizungumza kwa niaba ya Madiwani,Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo Mhe. Benjamini Sitta amesema kuwa mafanikio ya hati hizo safi zimetokana na usimamizi mahiri wa Mkurugenzi Ndugu. Aron Kagurumjuli pamoja na menejimenti kwani amekuwa mzalendo na kiongozi anayefuata sera na miongozo ya serikali.