Baadhi ya Ndugu wa Marehemu Christopher Mfinanga wakiongoza msalaba na picha yake kuelekea kanisa la KKKT Kibaha kwajili ya kuaga mwili wa Marehemu kabla ya kusafirishwa kijijini kwao Ugweno, Usangi Same mkoani Kilimanjaro.
Baadhi ya waumini waliyoshiriki Ibada ya kumuombea Marehemu Christopher Mfinanga katika kanisa la KKKT Kibaha kabla ya kusafirishwa kwenda kijijini kwao Ugweno, Usangi Same mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya safari yake ya mwisho.
Baadhi ya wananchi wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa Marehemu Christopher Mfinanga kwenye gari litakalo safirisha mwili huo kuelekea kijijini kwao Ugweno, Usangi Same mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya mapumziko yake ya milele.
Jeneza lililobeba mwili wa Marehemu Christopher Mfinanga likiingizwa katika gari tayari kwa kuelekea kijijini kwao Ugweno, Usangi Same mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya kumpumzisha.