Askofu Michael Msonganzila Jimbo Katoliki Musoma akiongoza ibada ya kumshuruku mungu kwa kulisaidia taifa kutokupata vifo vingi vya kutokana na virusi
vya Corona kama ilivyotabiriwa na mataifa ya nje katika Parokia ya Shirati, ambapo alisisitiza watanzania kuendelea kumuombea Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli ili azidi kukua na kuongezeka imani na busara katika kuliongoza taifa, jana Wilayani Shirati,Mkoani Mara.
Baadhi ya waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Shirati wakifuatilia ibada ya kumshukuru mungu kwa kuliepusha taifa na maambukizi na vifo vingi vya virusi vya Corona kama ilivyotabiriwa na mataifa ya nje iliyokuwa ikiongoza na Askofu Michael Msonganzila Jimbo Katoliki Musoma (hayupo pichani) jana.
Baadhi ya viongozi wa serikali ya wilaya ya Shirati na Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo wakiwa katika picha ya pamoja na Askofu Michael Msonganzila Jimbo Katoliki Musoma mara baada ya ibada ya kumshuruku mungu kwa kulisaidia taifa kutokupata vifo vingi vya kutokana na virusi vya Corona kama
ilivyotabiriwa na mataifa ya nje, jana katika Parokia ya Shirati, mwenye tisheti ya mistari ni Mkuu wa Wilaya ya Shirati Saimo Chacha,wa pili kushoto kwa waliyosimama
mbele ni Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni Dkt. Emmanuel Temu kuto Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo.
Baadhi ya Wazee wa Jadi Wilaya ya Rorya wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufanya tambiko la kuliombea taifa dhidi ya janga la virusi vya Corona wakiongozwa na Chifu wa eneo hilo Ngoje Ogati (watano kushoto) na mwenye tisheti ya mistari ni Mkuu wa Wilaya ya Rorya Saimo Chacha na (watatu kulia ni) Mkurugenzi
wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni Dkt. Emmanuel Temu kuto Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo jana.
*********************************
Na Anitha Jonas – WHUSM,Shirati
01/06/2020
Mara.
Watanzania tuendelea kumwombea Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli ili aendelee kukua na kuongezeka imani na busara.
Askofu Michael Msonganzila wa Jimbo Katoliki Musoma ametoa wito huo hivi karibuni katika ibada maalum ya kumshukuru mungu iliyofanyika katika Parokia ya Shirati kwa ajili ya kumshukuru mungu kwa kulisaidia taifa dhidi ya maambukizi ya Virusi vya Corona tofauti na ilivyotabiriwa na mataifa ya nje nah ii ni kufutia maono Mheshimiwa Rais yaliyosaidia taifa kukabiliana na janga la maambukizi ya Virusi vya Corona.
“Kwanini tung’ang’ane kupata taarifa za idadi za vifo, taarifa hizi hazisaidii sana bali zinaongeza hofu tu na pia hata taarifa za kweli zinapotolewa baadhi ya watu
wanabeza kwa Musoma hii mpaka sasa tunakifo kimoja tu cha mgonjwa wa Corona hakuna taarifa zinazofichwa Kanisa Katolikili lina mfumo wa kupata taarifa kuanzia
ngazi ya familia na tunafuatilia ” alisema Askofu Msonganzila.
Pamoja na hayo askofu huyo alieleza kuwa anafahamu katika kumshukuru mungu makundi mbalimbali ya imani tofauti yalifanya maombi yao na katika Wilaya ya Shirati
anafahamu kuwa wapo wazee wa kijadi katika eneo hilo nao walifanya tambiko.
Halikadhalika nae askofu huyo aliendeleea kusisitiza kuwa pamoja na idadi ya maambukizi kupungua lakini ni vyema wananchi wanaendelea kuzingatia ushauri wa wataalamu wa afya wa kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni, kuvaa barakoa na kuepuka msongamano.
Kwa upande wa Chifu wa Rorya Ngoje Ogati alisema kuwa tangu janga hilo la virusi vya Corona lilipotangazwa wazee wa eneo hilo kutoka koo mbalimbali walifanya tambiko la kuzuia ugonjwa huo usifike katika eneo lao na mpaka sasa hakuna mtu hata mmoja katika eneo hilo amepata virusi hivyo.
“Katika ibada yetu ya tambiko tuliyofanya hivi karibuni nilakuzuia maambukizi ya virusi vya Corona katika nchi yote kwa ujumla pamoja na kushukuru kwa eneo la Rorya
kutokupata maambukizi kabisa “alisema Chifu Ogati.
Nae Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni Dkt.Emmanuel Temu alishukuru uongozi wa Wilaya ya Rorya kwa kuruhusu makundi yote ya kiimani ikiwemo la wazee wa jadi kufanya ibada ya kushukuru na kuliombea taifa.
Halikadhalika nae mmoja wa wakazi wa Wilaya ya Rorya kutoka Kijiji cha Buturi Bi. Hudo Odemba alisema katika eneo lao hawajawahi kupata maambukizi ya virusi vya Corona na anaamini kuwa matambiko yaliyofanywa na wazee wa eneo hilo yamesaidia kuwakinga pamoja na taadhari wanazochukua za kunawa mikono kwa maji tiririka kila mara.