Home Mchanganyiko WIZARA YA MIFUGO YATOA VITENDEA KAZI KUBORESHA UCHUNAJI WA NGOZI

WIZARA YA MIFUGO YATOA VITENDEA KAZI KUBORESHA UCHUNAJI WA NGOZI

0

Mkurugenzi wa Uzalishaji na Masoko wizara ya Mifugo na Uvuvi Felix
Nandonde akimkabidhi vifaa vya uchunaji wa Ngozi kwenye machinjio ya
mkoa wa Arusha kwa ajili ya kuboresha Uzalishaji wa Ngozi Kaimu Katibu
tawala wa Mkoa huo David Lyamongi kwenye hafla iliyofanyika kwenye
ofisi za mkuu wa mkoa huo jijini Arusha picha zote na Ahmed Mahmoud
Arusha

………………………………………………………………………………………..
Na Ahmed Mahmoud,Arusha
Wizara ya mifugo na uvuvi imetoa vitendeakazi vya mazao ya mifugo kwa
wachunaji wa ngozi kwenye machiinjio yote ya mkoa wa Arusha kwa ajili
ya kuongeza thamani na kuboresha uchunaji wa Ngozi.

Akikabidhi vifaa hivyo kwa kaimu Katibu Tawala wa mkoa wa Arusha kwa
niaba ya wachunaji hao Mkurugenzi wa masoko na uzalishaji Felix
Nandonde alisema kuwa kwa kipindi kirefu ngozi zimekuwa  zikiharibiwa
ubora wake kwa matumizi ya vifaa visivyo na ubora.

kwa mujibu wa Nandonde wizara ilitoa mafunzo ya siku moja kwa
wachunaji wa ngozi mkoa wa Arusha ili kuboresha thamani ya Ngozi
ikiwemo kutoa leseni kwa kila mchunaji na vifaa hivyo kwa lengo la
kuongeza ubora kwenye kazi zao.

Alivitaja vitendea kazi hivyo kuwa visu vya kisasa ambavyo
vimetengezwa kwa teknolojia ya kisasa na vitatolewa bora kwa wachunaji
wa mkoa wa Arusha na nchini kwa ujumla

“Kwa kipindi kirefu sekta ya uchunaji nchini imekuwa ikionekana haina
mwenyewe lakini sasa kupitia serikali ya awamu ya tano imeanza
kutambulika kwa lengo la kuongeza mnyororo wa thamani wa mazao ya
mifugo”

Akiongea mara baada ya kupokea vifaa hivyo kaimu katibu tawala wa mkoa
wa Arusha David Lyamongi aliipongeza wizara hiyo kwa kutoa mafunzo kwa
wachunaji pamoja na vitendeakazi hivyo.

Aliongeza kuwa vitendeakazi hivyo vitawezesha mkoa huo kuzalisha ngozi
zenye ubora wa hali ya juu na hivyo ngozi zitakuwa na thamani kubwa na
masoko ya hali ya Juu.

Alisema kuwa mkoa wa Arusha ambao ni wa wafugaji vifaa hivyo vimekuja
wakati muafaka kusaidia kuondokana na matumizi ya vifaa butu ambavyo
vilikuwa vikitumika kuharibu ubora wa Ngozi na hivyo kuondoa thamani
yake.