Home Mchanganyiko TAS WAIOMBA SERIKALI KUANGALIA NAMNA YA KUWASAIDIA WATU WENYE UALBINO.

TAS WAIOMBA SERIKALI KUANGALIA NAMNA YA KUWASAIDIA WATU WENYE UALBINO.

0

*****************************

Na Farida Saidy,Morogoro

Chama cha watu wenye Ualbino Tanzania ( TAS) kimeiomba Serikali kuangalia upya sera na miongozo katika Sekta ya Afya ili kuwasidia watu wenye Ualbino katika upatikanaji wa vifaa kinga ikiwemo mafuta maalumu ya kujipaka ,kama ilivyo katika upatikanaji wa dawa za kufumpaza virusi vya Ukimwi ARV zinavyotolewa bure katika vituo vya Afya na Zahanati.

Kauli hiyo imetolewa Mkoani Morogoro na Katibu wa TAS Taifa Musaa Kabimba katika kliniki ya ngozi kwa watu wenye Ualbino, ambapo alisema anatambua mchango wa Serikali katika kuwasaidi watu wa kundi hilo lakini changamoto ni upatikanaji wa vifaa kinga kwani kumekua na gharama kubwa ukilinganisha na maisha yao, ambapo mafuta ya kujipata ili kujikinga na Saratani yanauzwa kuanzia Elfu 35 Hadi Elfu 40 jambo ambalo wengine wanashindwa kumudu bei hizo na kuiomba Serikali kuandaa utaratibu wa kuwapatia bure kama makundi megine.

Kwa upande wake Afisa Afya wa TAS Taifa Bwana Mohamed Chanzi alisema saratani ya ngozi ni miungonimwa magojnwa yanawapa changamoto watu wenye ualbino ambao asilimia kubwa ya wagonjwa wanaopatika na Saratani ya Ngozi wanakua wameathirika kwa kiwango kikubwa

Naye Daktari bingwa magonjwa ya ngozi amesema katika kuwasaidia watu wenye viashiria vya dalili vya saratani ya ngozi wanachomelewa na mionzi ili kupunguza uwezekano wa kupata Saratani huku afisa Ustawi wa Jamii Mratibu wa watu wenye ulemavu na Wazee Mansipaa ya Morogoor Rehema Malimi alisema Kati ya jitihada wanazozifanya katika kuwasaidia watu wa kundi hilo Ni pamoja na kulipatia elimu jinsi ya kujinginga wasipate maradhi mbalimbali.

Nao baadhi ya Baadhi ya Wazazi wenye watoto wenye Ualbino wamekishukuru chama hicho pamoja na Serikali katika kuwahakikishaia usalama watoto wao ukilinganisha na kipindi cha nyuma walikua wakiishi kwa hofu wakihofiausalama wa maisha yao.

Siku ya watu wenye Ualbino hufanyika kila ifikapao juni 13 kila mwaka lengo likiwa Ni kutoa elimu kwa jamii kuhusu watu wenye ualbino, ambapo mwaka huu kutokana na Ugonjwa wa Corona haitafanyika katika makundi Kama ilivyokawaida.